LICHA YA KUIFUNGA MAN UTD, CONTE BADO YUPO HATARINI

Licha ya kushinda dhidi ya Man Utd, Conte bado yupo hatarini

Dimba - - Front Page - LONDON, England

UAMUZI wa kocha wa Chelsea, Antonio Conte, wa kutomwanzisha beki wake, David Luiz, kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya Man United huenda ukamharibia Muitaliano huyo, historia inaonesha hivyo. Mchambuzi wa Sky Sports, Gary Neville, alifafanua hilo kwa kusema katika miaka ya hivi karibuni, pindi hali inapokuwa si shwari Stamford Bridge, basi ni mmoja tu atakayeshinda vita. Ilibainika kuwa, Luiz na kocha wake huyo walitofautiana kauli mazoezini baada ya beki huyo kuhoji juu ya mbinu zake, swali lililopokelewa kwa mtazamo tofauti na ndipo alipoamriwa afanye mazoezi kivyake kabla hawajavaana na Man United wikiendi iliyopita.

“Alichokifanya Conte si kitu kidogo, mara nyingi makocha waliowahi kuwepo Chelsea hawakudumu kwa muda mrefu. Alichokifanya kwa mchezaji kama Luiz ambaye ana ushawishi mkubwa kwa wenzake kinaweza kuigharimu kazi yake. Huu si mwisho, huu ndio mwanzo wa balaa.

“Bahati yake ni kwamba alishinda dhidi ya United, lakini kama Luiz akiendelea kukaa benchi kwa wiki mbili au tatu na wakaruhusu bao kila mara, lazima kamera zielekezwe kwa Luiz. Ni sawa na ilivyokuwa kwa John Terry,” alisema Neville.

Gary Neville

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.