Samatta hatihati kuikosa Benin

Dimba - - Jumatano - NA JESSCA NANGAWE

STRAIKA anayecheza soka la Kimataifa, Mbwana Sammata, ana hatihati ya kuukosa mchezo wa kimataifa dhidi ya Benin, utakaochezwa Jumamosi hii nchini humo.

Kikosi cha Stars chenye wachezaji 24 kinatarajia kuondoka kesho kuelekea Benin tayari kwa mchezo huo, huku wachezaji wa kimataifa wakitarajia kuungana na timu wakiwa huko.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, aliliambia DIMBA kuwa wamefanya mzungumzo na wachezaji hao ambao watajumuika na timu huko Benin, huku taarifa za kuumwa za straika huyo wakizipata lakini akidaiwa kuwa na majeraha ya kawaida.

"Tunatarajia timu itakwenda Benin Alhamis na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa, Mbwana Samatta, Farid Mussa pamoja na Abdi Banda wakitarajiwa kuungana na timu huko, kwa mujibu wa madaktari wanaomtibu Samatta wamekiri kuwa mchezaji huyo ni majeruhi wa kawaida, hivyo huenda akacheza ama asicheze," alisema Alfred.

Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, anadaiwa kuumia goti Jumamosi iliyopita wakati timu yake ikicheza na Lokeren na timu hizo kutoka suluhu ya 0-0, katika Uwanja wa Luminus Arena.

Stars na Benin inakutana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.