Hawa wanadaiwa chenji Simba, Yanga

Dimba - - Jumatano - NA CLARA ALPHONCE SAID MOHAMED 'NDUDA' JAMAL MWAMBELEKO EMMANUEL MSEJA ABDALLAH SHAIBU 'NINJA' BARUANI YAHYA

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imefikia mzunguko wa tisa, klabu za Simba na Yanga zinaongoza kwa kuwa na wachezaji waliosajiliwa kwa gharama kubwa, lakini hawajatumika ipasavyo ambao kwa lugha ya kimjini mjini wanajulikana kama wanaodaiwa 'chenji.'

Klabu ya Simba kwa maelezo yao wametumia zaidi ya Sh bilioni 1.3 za usajili, lakini baadhi yao mpaka sasa wanakula bata tu wakiwa hawatumiki, huku Yanga nao wakiwepo wachache wakiwa kama watazamaji tu.

Wakati Simba wao wakisema walitumia kiasi hicho cha fedha kwa usajili, Yanga wao hawakuweka bayana kiasi walichotumia ila inakadiriwa kuwa si chini ya Sh milioni 500, kubwa wakilenga michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na ile ya kimataifa, ambapo watashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kutokana na hali hiyo, kwa kauli rahisi unayoweza kusema wachezaji hao ni kama wanadaiwa chenji na timu zao hizo, kwani hawajazitumikia ipasavyo licha ya kwamba ligi bado mbichi, kwani ni michezo tisa iliyokwishakuchezwa mpaka sasa kati ya 30 ambayo kila timu inapaswa kuicheza.

Kwa upande wa Simba, kundi la wachezaji ambao hawajaitumikia kabisa klabu hiyo linaongozwa na Shomary Kapombe ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili ndani ya Simba wenye gharama ya Sh milioni 40, lakini mpaka sasa kashindwa kucheza kutokana na kusumbuliwa na majeruhi aliopata kabla ya msimu huu kuanza.

Kipa namba mbili aliyesaini mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo kwa Sh milioni 30 akitokea Mtibwa Sugar, lakini ameshindwa kuzitumikia fedha hizo kutokana na majeraha ambayo aliyapata wakati wa maandalizi ya mwanzoni mwa msimu.

Mlinzi wa kushoto amesajiliwa kwa dau linalokadiriwa kuwa Sh milioni 25 na alisajiliwa kwa ajili ya kumpa changamoto Mohammed Hussein 'Tshabalala’ ambaye alionekana hana mbadala kwenye nafasi anayocheza.

Mlinda mlango huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili, ameshindwa kupata nafasi mbele ya Aishi Manula na kama akipona Said Mohamed, hali ya kinda huyo inaweza kuwa mbaya zaidi kwani atakuwa chaguo la tatu kama hatajibidiisha.

Kwa upande wa Yanga wanaongozwa na Amis Tambwe ambaye licha ya kuongozewa mkataba wa miaka miwili, bado hajatumika katika mchezo wowote tangu msimu huu kuanza kutokana na majeraha yanayomkabili.

Ni beki wa kati aliyesajiliwa kutoka Zanzibar, lakini hali inaonekana kumuwia ngumu kutokana na uwepo wa Kelvin Yondani na Andrew Vincent, ambapo ameishia tu kucheza mechi za kirafiki lakini mguu wake haujagusa mchezo wowote wa ligi kuu.

Alisajiliwa Yanga akitokea Mtibwa Sugar kwa ajili ya kuziba nafasi ya Simon Msuva ambaye amekwenda kucheza soka Uarabuni, lakini ameshindwa kufanya hivyo na kuambulia kukaa benchi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.