Chaneta yadaiwa mil 7/- za ada

Dimba - - Jumatano - NA ZAINAB IDDY

CHAMA cha Netiboli Tanzania (CHANETA), kinasaka kiasi cha dola 3250 zikiwa sawa na zaidi ya Sh mil 7,81,520 kwa ajili ya kulipa ada ya uanachama wake kimataifa.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Mwenyekiti mpya wa Chaneta, Devoth Marwa, alisema deni hilo wamelikuta baada ya kuingia madarakani.

Alisema Chaneta inadaiwa kiasi cha dola 2250 (Sh mil 4,991,710) ambayo ni ada ya miaka mitatu katika Shirikisho la Kimataifa (IFNA) na penalti dola 500 (Sh mil 1,104,850), lakini pia ada ya dola 500 (Sh mil 1,104,850) ambayo ni ada ya miaka miwili kwa shirikisho la mchezo huo Afrika jumla ikiwa mil 7,181,520.

“Kwa sasa tupo katika mchakato wa kutafuta fedha hizo ili tuweze kulipa madeni hayo na kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa ambayo yanasaidia kupandisha viwango kimataifa,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.