Daba kuanza na timu ya vijana

Dimba - - Jumatano - NA WINFRIDA MTOI

BAADA ya kufanikiwa kutetea kiti chake, Mwenyekiti wa Chama cha Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es Salaam (DABA), Akaroly Godfrey, amesema wanarejea na kasi mpya kwa kuanzisha timu ya vijana ya kudumu.

Akizungumza na DIMBA Jumatano jana, Godfrey alisema anaamini wadau wa ngumi wameamini utendaji wake na kumpa nafasi hiyo kwa mara nyingine, hivyo hatawaangusha na atakuja na mikakati mingi ya kukuza mchezo huo.

“Nashukuru kwa kupata nafasi nyingine, kama uongozi wa Daba tunaandaa mikakati imara ya kukuza mchezo huu kuanzia ngazi za chini na tutaanza na timu ya vijana ya mkoa,” alisema.

Kipa wa timu ya Vijana wanaolelewa na Klabu ya Simba, Halfan Romanusi, akiokoa moja ya shambulizi lililopigwa golini kwake wakati wa mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam jana. Picha na John Dande

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.