Nyamwela aikingia kifua dansi

Dimba - - Jumatano - NA JESSCA NANGAWE

MNENGUAJI mkongwe wa muziki wa dansi, Hassan Musa ‘Super Nyamwela’, amesema pamoja na muziki huo kuonekana kupotea njia, lakini amesisitiza bado wanaweza kuurudisha kwenye hadhi yake.

Akizungumza na DIMBA, Nyamwela amesema muziki huo umeshindwa kutangazwa na wasanii wenyewe na ndiyo maana umeonekana kukosa soko kama ilivyokuwa awali. “Unajua miaka ya sasa sisi wenyewe ni kama tumeuroga muziki wetu, haupati matangazo ya kutosha kwa maana ya kuutangaza kama zamani na tumeonekana kuridhika na hali hii, nadhani kikubwa tuamke, tupambane na kushirikiana katika kuhakikisha tunarudisha soko lake,” alisema Nyamwela. Kwa sasa msanii huyo anafanya vizuri na kibao chake kipya cha ‘Kochokocho’, chenye mahadhi ya Bongo Fleva na dansi alichokitoa hivi karibuni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.