Baraka De Prince

alia na hujuma mitandaoni

Dimba - - Jumatano - NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Baraka De Prince, amefunguka na kudai kuna watu wanamfanyia hujuma kupitia nyimbo zake ili apotee kimuziki.

Baraka, ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya Sometimes, amesema kuna watu wameamua kuchezea mtandao wa youtube na kufanya ngoma yake mpya ya ‘Sometimes’ isionekana na kusisitiza endapo watafahamika, anaomba sheria kali zichukuliwe dhidi yao.

“Nimekuwa nikiandamwa sana na wengi wakidai nimepoteza mwelekeo, wameona haitoshi wamekwenda kuzuia wimbo wangu usionekane kwenye mtandao wa youtube, nadhani hii ni kutaka kuniharibia, wajue tu hawataweza,” alisisitiza Baraka.

Aidha, Baraka amesisitiza kuwa, tayari amefikisha taarifa hizo kwenye vyombo husika na wakati wowote vyombo vya sheria vitawachukulia hatua za kisheria wahusika.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.