NA SHARIFA MMASI

Dimba - - Jumatano -

MSANII anayeendelea kufanya vema kwenye tasnia ya muziki wa RnB, Benard Paul, maarufu ‘Ben Pol’, amesema mbali na kazi ya sanaa anayojishughulisha nayo, yeye ni mkulima wa mazao aina tofauti tofauti. Akizungumza na DIMBA jana, Ben Pol alisema ameajiri vijana mbalimbali kwaajili ya kusimamia shughuli hiyo. “Wengi hufahamu maisha ya Ben Pol yanategemea muziki peke yake, lakini haikuwa hivyo, kwani mimi ni mkulima wa mazao mbalimbali,” alisema Ben Pol. “Katika kuhakikisha nasaidia vijana wenzangu, nimeajiri wafanyakazi ambao nawalipa gharama kwaajili ya kusaidia shughuli nzima za shambani,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.