TETESI ZA MASTAA ULAYA

Dimba - - Jumatano -

RONALDO OUT, NEYMAR IN

IMERIPOTIWA kuwa Rais wa Klabu ya Real Madrid, Florentino Perez, alikutana na baba wa mshambuliaji wa PSG, Neymar, kwa ajili ya mazungumzo juu ya uwezekano wa kumrudisha staa huyo Hispania kuchukua nafasi ya Cristiano Ronaldo.

BEKI ATAKIWA CHELSEA

MABINGWA watetezi wa Premier League, Chelsea, wanafikiria suala la kumsajili beki wa Lyon, Mouctar Diakhaby, 20, ambaye yupo pia kwenye rada za klabu ya Manchester City.

VALENCIA YAOMBEA PEREIRA ASICHUKULIWE

KLABU ya Valencia ina matumaini kuwa klabu ya Man Utd haitamchukua kiungo wao, Andreas Pereira, aliye katika timu yao kwa mkopo kutokana na kiwango safi alichokionesha hadi sasa, kwa kufunga bao moja na kutoa asisti tatu katika mechi 10 za La Liga.

MAX MEYER ANUKIA SPURS

KIUNGO mshambuliaji anayekuja kwa kasi hivi sasa, Max Meyer wa Schalke, huenda akawa mchezaji wa kwanza kutua Tottenham katika dirisha la usajili wa majira ya kiangazi, kwani timu hiyo ya England bado inamfukuzia kwa kasi.

ARSENAL YAMNYATIA NAVAS

WASHIKA mitutu wa London, Arsenal, wanataka kumsajili mlinda mlango wa klabu ya Real Madrid, Keylor Navas, ambaye anahusishwa kutakiwa na Liverpool. Na wakati huo huo, Arsenal wamefufua harakati zao za kumtaka kiungo wa Barcelona, Rafinha, 24.

PSG WAIFUKUZIA SAINI YA MORATA

TETESI ya motomoto ni kwamba Paris Saint-Germain inataka kumsajili straika wa Chelsea, Alvaro Morata, kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Edinson Cavani. Kwa mujibu wa mtandao wa Marca, Cavani anatarajiwa kuikacha PSG Julai, mwakani huu, sababu kuu ikidaiwa ni ugomvi wake na Neymar.

LUKE SHAW ATAFUTWA NA WATURUKI

BEKI wa kushoto wa Man Utd, Luke Shaw, amenasa kwenye rada za Fenerbahce, kwa mujibu wa ripoti zilizopo Uturuki. Shaw, 22, hajacheza mechi yoyote ya Premier League msimu huu na ametajwa kuwa ataondoka Januari.

YAYA TOURE KUTIMKIA MAREKANI

MKONGWE wa Ivory Coast na kiungo wa Manchester City, Yaya Toure, ameripotiwa kuwa huenda akaenda kumalizia soka lake kwenye Ligi Kuu nchini Marekani, mara baada ya kumaliza mkataba wake na 'The Cityzens.'

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.