KWA MAN CITY ILE, MOURINHO ANAFUKUZA UPEPO TU

Dimba - - Jumatano - NA BADI MCHOMOLO Tukutane wiki ijayo, Maoni na Ushauri nicheki kwa namba 0714107464 au Email Badimchomolo@ yahoo.com

TOLEO la wiki iliyopita tuliona jinsi Mayweather alivyokuwa na furaha baada ya baba yake kumwambia kwamba, yupo tayari kwa kushiriki mapambano hivyo akae tayari.

Alipewa nafasi hiyo baada ya kuchukua maamuzi ya kupiga watu mitaani ili kupeleka kesi kwa baba yake na aweze kumpa nafasi ya kushiriki mashindano.

Ikumbukwe kwamba baba yake aliamini kuwa Mayweather bado hana uwezo wa kushiriki mashindano, kwa kuwa alikuwa hawezi kumshambulia mpinzani, lakini alikuwa na uwezo wa kujilinda.

Kutokana na vitendo hivyo vya kupiga watu, baba yake alimwambia muda wake umefika wa kuanza kushiriki mashindano, hivyo akae tayari.

Huku Mayweather akiwa na furaha hiyo mwaka 1992, baba yake alikamatwa na polisi kwa tuhuma za biashara ya dawa za kulevya.

Hapo ndipo Mayweather alianza kukata tamaa ya kushiriki mashindano yoyote ya ngumi kwa kuwa baba yake ambaye ndio mwalimu wake amewekwa ndani.

Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa bingwa huyo wa ngumi, hapo ilifikia hatua ya kutaka kuachana na mchezo huo huku akiangalia hali ya mama yake ambaye ameathirika na dawa za kulevya anazidi kuchanganyikiwa.

Ikumbukwe kwamba shangazi wa Mayweather alipoteza maisha baada ya kuathirika na dawa za kulevya na baadaye kupata virusi vya Ukimwi, huku mama yake hali yake ikiwa inasikitisha mitaani.

Bahati ambayo alikuwa nayo Mayweather ni familia yake ina watu wengi ambao wanajua kucheza ngumi na kwa wakati huo walikuwa walimu wa mchezo huo wakishirikiana na baba wa Mayweather, kama vile Jeff Mayweather ambaye alikuwa bingwa wa mkanda wa IBO na Roger Mayweather ambaye alikuwa bingwa wa WBA na WBC.

Wakati huo Mayweather anafikiria kutaka kuachana na ngumi kutokana na baba yake kufungwa, wajomba zake hao wawili walimhakikishia anapata pambano.

Bado hakuwa na imani sana kwa kuwa alimini baba yake alikuwa kila kitu katika maisha yake, lakini wajomba hao walimtaka kuondoa wasiwasi na walianza kuwa naye karibu ili kumpunguzia mawazo na kumpa mazoezi ya nguvu.

Mayweather alikubali kuendelea na ngumi lakini kwa shingo upande, lakini kila wakati aliwasisitizia kwamba anahitaji pambano ili ajipime.

Miezi michache baadaye kabla ya Mayweather kupewa pambano, baba yake anatoka katika kifungo chake, hivyo Mayweather alikuwa na furaha kubwa na alitaka kumuonesha baba yake kuwa tayari amewiva, hivyo aliwaomba wajomba wampe pambano ili amuonesha baba yake, lakini baba alikataa na kusema anatakiwa akae naye mwezi mmoja ili kuangalia kama ana uwezo huo.

Baada ya mwezi kumalizika, baba alikubali kiwango cha mtoto wake, hivyo alimwambia sasa upo tayari kushindana, kikubwa ni kuwa na heshima ya mchezo, unajua alipangiwa kupigana na nani kwa mara ya kwanza katika ushindani?

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.