UNA HABARI?

NA MAREGES NYAMAKA

Dimba - - Jumatano -

CHIRWA NA KASEKE WALIVYOKAMATIKA

UKIAMBIWA wachezaji wakati mwingine wana akili ya ziada kupata matokeo kwa kuwahadaa waamuzi, inakubidi ukubaliane na hili, hilo lilitokea mwishoni mwa wiki kati ya Deus Kaseke wa Singida United na Obrey Chirwa kutoka Yanga. Alikuwa ni Kaseke aliyeonekana kumdanganya mwamuzi kuwa amefanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari, lakini baada ya janja hiyo kumsaidia, kilichomkuta ni kuonyeshwa kadi ya njano na dakika chache baadaye Chirwa akakumbana na tukio kama hilo.

MASHABIKI WA MBEYA BADO WAZING’ANG’ANIA SIMBA, YANGA

BILA shaka bado unakumbuka jinsi mashabiki wa timu ya Mbeya City walivyolalamikia bao walilofungwa timu yao na kikosi cha Simba Jumapili iliyopita. Basi kama huna habari hivi sasa mashabiki hao wameamua kuzikamia vilivyo hizi timu kongwe Simba na Yanga, ambapo mikakati iliyopo kwa sasa ni kuhakikisha Simba inapoteza mchezo wake dhidi ya Tanzania Prisons na Yanga inapata kipigo kutoka kwa Mbeya katika mechi zitakazopigwa Novemba 18 na 19

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.