MAJIBU YA WIKI ILIYOPITA

Dimba - - Jumatano -

Wiki iliyopita kulikuwa na mada inayozungumzia juu ya uwezo wa kiungo mkabaji wa Yanga, Mkongomani Papy Kabamba Tshishimbi, kwenye kikosi cha Yanga kwa sasa je, umemaliza tatizo la namba sita kwenye timu hiyo?

Yanga ambao walikuwa wanasumbuliwa na tatizo la kiungo mkabaji kwa muda mrefu, kwa sasa tangu asajiliwe Mkongo huyo, amekuwa akionyesha kiwango kizuri na kuteka hisia za mashabiki na wadau wengi wa soka nchini.

Kutokana na hilo, wadau wengi waliotuma maoni yao juu ya suala hilo wameeleza kuwa, ni kweli kwa sasa Yanga tatizo la kiungo limepungua na huenda likaisha kabisa kutokana na kupata viungo wazuri akiwemo Tshishimbi, Raphael Daud na Pius Buswita.

Naitwa Julius Nyakibar kutoka Ilemela Mwanza, kiukweli Tshishimbi kamaliza kiu ya kiungo mkabaji Yanga.

Naitwa Said Mussa wa Masasi, Tshishimbi bado inaonyesha anapokutana na Simba huwa anakamia zaidi kuliko timu nyingine, anatakiwa kuonyesha uwezo katika kila mechi.

Naitwa Denis Kulinga wa Mbeya, kwa ujumla kiungo Papy Tshishimbi kaonyesha uwezo katika kikosi cha Yanga na ataisaidia sana timu hiyo.

Niatwa Noel Steven wa Gongolamboto, Papy Tshishimbi amekata kiu ya Wanayanga ya kiungo mkabaji.

Naitwa Peter Nguni wa Nyasa Songea, kweli Tshishimbi amemaliza tatizo la kiungo kwenye kikosi cha Yanga.

Naitwa Mbiti Magibo wa Dar, huyu Tshishimbi ni habari nyingine kabisa pale Yanga na hata ameweza kufanikiwa kuwasahaulisha habari za Niyonzima na kumaliza tatizo la kiungo mkabaji.

Naitwa Andrew Mwanda wa Kyela, katika mwaka ambao tumebahatika suala la usajili wa viungo ni mwaka huu, kwani imepata viungo wazuri kama Tshishimbi, Buswita na Raphael Daud.

Naitwa Juma Mrutu napatikana Same, kama Tshishimbi hataandamwa na majeraha na akiendelea na kiwango chake alichokionyesha tangu amekuja, basi Yanga itakuwa nzuri sana eneo la kiungo. Mimi ni Adini Chama wa Tunduru, kwa kweli Yanga sasa tatizo la kiungo limepungua na huyu Tshishimbi anatisha sana, nampongeza.

Naitwa Regan Watanabe wa Arusha,Yanga wamelamba dume kwa sehemu ya kiungo, kwani Tshishimbi anamudu vema nafasi yake.

Naitwa Shoham Maliga wa Iringa, naona tatizo la kiungo pale Yanga limekwisha kwa kuwa amepatikana Tshishimbi, kwani anajua kumiliki dimba la kati vizuri.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.