Evergreen yatamba kutwaa ubingwa

Dimba - - Jumapili - NA GLORY MLAY

KOCHA wa timu ya soka ya Evergreen, Omari Nyango, amesema hawatakubali kuona ubingwa unachukuliwa na timu pinzani katika michezo ya Ligi Kuu, itakayoanza Novemba 26, mwaka huu, katika vituo viwili vya Dar es Salaam na Arusha.

Akizungumza na DIMBA jana, Nyango alisema kikosi chake kinaendelea na mazoezi makali pamoja na mechi za kirafiki kuhakikisha wanatwaa ubingwa msimu huu.

“Tumeshaanza mazoezi kujiandaa na mashindano ya Ligi Kuu, pia wachezaji wote wapo fiti katika kukabiliana na ushindani,” alisema.

Timu ya Evergreen imepangwa katika kundi A, zikiwamo timu ya Simba Queens, Mburahati Queens, JKT Queens, Fair Play ya Tanga na mabingwa watetezi Mlandizi Queens.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.