Oklahoma City yaichapa Los Angeles Clippers vikapu 120-111

Dimba - - Jumapili - OKLAHOMA, MAREKANI

TIMU ya kikapu ya Oklahoma City Thunder imeibuka na ushindi wa vikapu 120 dhidi ya 111 vya Los Angeles, mchezo uliopigwa katika dimba la Chesapeake Energy Arena.

Oklahoma wanashika nafasi ya 12 mara baada ya michezo hiyo ambapo wameshinda mara tano pekee huku wakipoteza mara saba.

Mchezo huo wa kanda ya Magharibi vijana hao wa Billy Donovan, walikuwa katika ubora wa aina yake katika mtanange huo ambao, Paul George, alifunga vikapu 42.

Huu ulikuwa mchezo wa kwanza wa George kufunga vikapu vingi tangu alipojiunga na Thunder mwishoni mwa msimu uliopita.

Russell Westbrook alifunga vikapu 22 huku akitoa pasi nane za mabao, Carmelo Anthony pamoja na Alex Abrines kila mmoja alifunga mara 14.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.