He! Kumbe Neymar mtata toka zamani

Dimba - - Jumapili - PARIS, UFARANSA

TANGU atue PSG akitokea Barcelona kwa uhamisho wa euro mil 221 ulioweka rekodi ya dunia, Neymar amekuwa na matukio yasiyoeleweka.

Awali nyota huyu wa Brazil, aligombana na mchezaji mwenzake, Edinson Cavani, walipogombea kupiga penalti, PSG ilipoichapa Lyon, mabao 2-0.

Lakini hivi sasa ameibua mgogoro mwingine na kocha wa PSG, Unai Emery, kwa madai ya kutofurahishwa na mbinu za mwalimu huyo, hali inayomfanya achague mechi za kucheza.

Inadaiwa kuwa Neymar amekuwa akijitoa zaidi kwenye michezo ya Ulaya na hurudi kucheza chini ya kiwango katika mechi za Ligue 1. Ni kisirani kweli kweli!

Wanaomjua vizuri Neymar watakuwa wanajua kuwa hii si mara ya kwanza kwa Mbrazili huyu kugombana na makocha pindi anapotaka jambo lake lifanyike.

Akiwa na klabu ya Santos ya Brazili, Neymar aliwahi kugombana na kocha wake, Dorival Junior, baada ya kunyimwa asipige penalti katika mchezo dhidi ya Atletico GO.

Ugomvi huu uliendelea na baadaye kocha Dorival, alijikuta akitupiwa virago na viongozi wa Santos.

"Siko hapa kwa ajili ya kujitetea," alisema Neymar baada ya tukio hilo. "Nimekuja kuwaomba msamaha wale wote wanaofurahia mchezo wa soka. Neymar halisi si yule mliyemwona jana. Mimi ni mtu safi, mcheshi ninayependa kucheza na tabasamu usoni. Nilirudi nyumbani na kutazama kilichotokea, nilijisikia vibaya sana."

Imekuwa kawaida kwa Neymar kuomba msamaha pindi anapofanya tukio la hovyo, lakini si kwamba huwa anaacha.

Mbali naugombana na wachezaji wen, zake wa Barcakabla hajatimkia Nou Camp, taarifa za ndani ya klabu hiyo zinadai kuwa Neymar alikuwa kwenye mgogoro na benla chi la ufunndklabu hiyo.

"Alikuwa akiwachukia makocha wote," chanzo chahabari kiliupasha mtandao wa Goal. "Tangu akiwa Santos, alikuwa na kawaida ya lugombana na walimu, hasa katika maamuzi ya nani acheze na nini anaa takiwa kufanya uwanjani.

"Hapa Barca alikuwa akikerwa na mbinu za Luis Enrique, mara nyingi alimbia kuwa akimwambia nini cha kufanya na ni wachezaji gani wanatakiwa kufanyiwa mabhuu adiliko.

"Ugomvi ukampelekea kocha msaidizi wa Barca, Unzue, kumtahadharikuwa sha Neymar makini na tabia zake vinginevyo atamaliza soka lake kama Ron Ugomvi aldinho."

na Neymar na Emery unatajwa kuanza baada ya Mbrazil huyu kugomea mbinu za kufundishwa kwa mikanda ya video, hali inayomfanya ashindwe kuhudhuria maandalizi ya baadhi ya mechi.

Uhasama huu wa Unai na Neymar umekuwa mkubwa ambapo sasa baadhi ya Wabrazili wanaokipiga katika klabu ya PSG, kuanza ujeuri kwa kocha huyo.

Dani Alves amegombana na Cavanni, huku Wabrazili wengine wawili, Thiago Silva na Lucas Moura, rafiki wa karibu na Neymar ambaye mpaka sasa hajaanza kwenye mchezo wowote wa Ligue 1, wakitishia kuondoka klabuni hapo.

Je, ni kweli Neymar hana furaha katika Jiji la Paris? Dalili zote zinaashiria hivyo. Nini kitafuata? Unai ataondoka au Neymar atahama na jeshi lake kusaka malisho sehemu nyingine? Wakati utatupa majibu sahihi katika hili.

JOHN TERRY

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.