Acheni vichwa vya makocha vifanye mambo dirisha dogo

Dimba - - Jumapili -

TUKO katika msimu wa usajili wa dirisha dogo, ni kipindi muhimu sana kwa timu kujaribu kujiweza sawa, kabla ya kiuendelea tena kupigania nafasi yoyote katika michuano hii ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hiki ni kipindi chenye sehemu mbili, yani kucheka na kulia iwe kwa makocha au wachezaji, pia ndiyo kipindi cha majuto kama timu itakichezea vibaya maana hakuna muda mwingine wa kujiimarisha zaidi ya huu.

Wito wangu ni aina ya mapokeo ya kipindi hiki, mara nyingi timu zinaangalia mapungufu hilo halina siri, na kwa kawaida anayejua udhaifu wa timu au mchezaji ni Kocha ambaye ndiye anayeishi na wachezaji kwa asilimia 90 ukioandoa muda wanaokwenda kupumzika.

Huyu ndiye anayejua hili au lile, wapi palipwaya na sehemu ipi ilikaza sana, hivyo jukumu la kujenga upya huwa linamuhusu kwa asilimia kubwa.

Japokuwa siyo jambo jema kusafiri kwa historia au kukariri lakini huko nyuma, tumeona baadhi ya timu zilizoingia katika mgogoro na pengine kushindwa kutimiza malengo baada ya kuichezea kipindi kama hiki.

Wapo makocha tena wengine wa kigeni na wenye sifa lukuki na taaluma ya kutosha katika ufundishaji wa soka duniani, lakini walijikuta wakishindwa kutimiza malengo pale walipokosa nafasi ya kufanya ushaurfi juu ya usajili.

Waliaminishwa nao wakaamini kwamba, maneno matamu ya viongozi yanayotaja majina ya wachezaji yanaweza kupata tafsiri ya ufanisi viwanjani, kumbe wakajikuta wanaingia katika mtengo wa kusajili vijeba na wachezaji wasiokuwa na vigezo hata vya kucheza ligi daraja la nne, matokeo yake ni kuingia hasara na pia kuzigharimu timu kukosa nafasi waliyostahili.

Mara nyingi inapokaribia tarehe kama hii ijayo yani 15, Novemba siku ambayo dirisha dogo litafunguliwa huwa nimejiwekea utaratibu wa kuyatunza maneno yangu haya katika ukurasa huu, ambayo hata yakiuonekana yamechakaa na kupitwa na wakati, lakini baada ya matukio kushabihiana maneno haya yanakuwa mapya na yenye harufu ya utuli badala ya uvundo kama yanavyoweza kuchukuliwa katika kipindi hiki.

Nawaombea nafasi ya ushiriki wa mawazo kama siyo vitendo makocha wote wanafundisha soka katika nchi yetu, wapewe fursa ya kuwa washiriki katika uundwaji wa timu, ili kesho na kedshokutwa tupate sababu ya kuwauliza endapo kile mlichokipanga pamoja hakikufikia malengo.

Ni jambo jema klabu zikaitumia nafasi hii hata kuweka sawa adabu za wachezaji hata kama walicheza vizuri katika michuano hiyo kwani kama walikosa ustaarab basi pia ni mapungufu ambayo katika soka huwa yanaigharimu timu.

Wapewe nafasi wenye uwezo lakini pia waliotimia kinidhamu, hiyo ndiyo Rai ya beki wenu mkongwe wa kulia. Amri kwa sasa ni kocha anayeifundisha timu ya Lipuli ya Iringa. Anapatikana kwa simu namba 0659 997 979

BEKI WA KULIA AMIR SAIDI - 0774 132 999

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.