Kipigo chamwibua kocha Bafana

Dimba - - Jumapili - POLOKWANE, AFRIKA KUSINI

KOCHA Stuart Baxter (pichani), anayeifundisha timu ya taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana), amesisitiza kwamba wamekosa nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa sababu walikosa bahati na si kitu kingine.

Kauli hiyo ambayo inaelezwa kuwa ni utetezi, imetolewa na kocha huyo saa chache baada ya kikosi chake kukubali kipigo cha mabao 2-0 ilipoikaribisha Senegal mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Peter Mokaba mjini Polokwane, ijumaa iliyopita.

"Tumepoteza kwa sababu tu hatukuwa na bahati, naamini tunaweza kufika mbali kwenye mechi zijazo kwa maana ya michuano mingine lakini kwa sasa inafaa tujipange upya na kuandaa timu yetu upya.

Bafana Bafana ilihitaji kushinda kwenye mchezo huo ili kuwa na uhakika wa kupata nafasi hiyo lakini kipigo hicho kimeifanya kupoteza nafasi hiyo ambayo imetwaliwa na Senegal huku timu zote zikiwa zimebakisha mchezo mmoja mkononi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.