Henry Onyekuru ataka majukumu zaidi Nigeria

Dimba - - Jumapili - LAGOS, Nigeria

STRAIKA wa kimataifa wa Nigeria, Henry Onyekuru (pichani), ametangaza kwamba anahitaji kupewa majukumu makubwa zaidi katika timu yake ya taifa kwa sababu ni sehemu ambayo alikuwa akiitarajia kuifanya kwa muda mrefu ambapo sasa ndoto zake zimetimia.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, amesema kupitia mtandao wake wa twitter kwamba dhamira yake ni kuona anapata nafasi kubwa na kupewa majukumu makubwa zaidi katika kikosi cha Nigeria maarufu kama Super Eagles.

"Nimepata nafasi kwenye timu ya taifa, nashukuru kwa kupewa imani kubwa lakini bado nahitaji kupewa makujumu makubwa zaidi kwa siku zijazo," alisema nyota huyo anayecheza katika klabu ya Everton ya England kwa mkopo akitokea RSC Anderlecht ya Ubelgiji.

Pamoja na kauli ya nyota huyo, lakini baadhi ya vyombo vya habari vya Nigeria vimesema kwamba lazima Onyekuru aongeze juhudi ili kumshawishi kocha wake awepo kwenye kikosi cha mwakani kitakachoshiriki Kombe la Dunia kutokana na ushindani uliopo ndani ya timu. Katika mchezo uliopigwa Ijumaa usiku, Nigeria ilipata sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Algeria iliyokuwa mwenyeji.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.