Baada ya Aslay sasa zamu yangu Enock Bella:

Dimba - - Jumapili - NA SHARIFA MMASI

MSANII wa Bongo Fleva, Enock Bella, ameweka wazi juu ya ukimya aliokuwa nao kabla ya kuachia wimbo wake mpya wa ‘Sauda’, badala yake alitoa nafasi kwa wenzake akiwamo Aslay kutamba sokoni. Akizungumza na DIMBA jana, Enock alisema sasa imeÀka zamu yake ya kuteka soko la Bongo Fleva sambamba na kujitengenezea mazingira ya kupata shoo ndani na nje ya nchi. “Ukimya wangu hapo awali haukutokana na kufulia kama namna watu walivyokuwa wakiyasema, badala yake nilitoa nafasi kwa wenzangu kina Aslay wajitengenezee mazingira ya sokoni na kupata shoo. “Nimeona huu ni wakati mwafaka kuwapa mashabiki wangu kile walichokuwa wakikisubiri kwa muda mrefu, naamini wimbo wangu mpya utaniweka katika mazingira mazuri kupaa kimataifa,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.