Dansa Twanga Pepeta ageukia Bongo Fleva

Dimba - - Jumapili - NA MAREGES NYAMAKA

MNENGUAJI wa bendi ya Twanga Pepeta, Hamza Mapande ‘Dogo White’, amegeukia upande wa pili na kuingia studio kuimba muziki wa Bongo Fleva na anatarajia kuutambulisha wimbo wake mpya Alhamisi ya wiki ijayo.

Dogo White aliliambia Dimba kuwa ameangalia fursa katika tasnia ya muziki na kuamua kujiongeza kutumia kipaji chake kingine cha uimbaji kuhakikisha anaendelea kuwapagawisha mashabiki wake kwa pande zote mbili kama mnenguaji na mwimbaji.

“Unajua nimeingia kwenye muziki muda mrefu sana, ni muda kwa wapenda burudani kusikia sauti ya dhahabu, naamini sitawaangusha kwani wimbo wangu huu uitwao ‘Mrembo’ utakonga nyoyo za walio wengi, wakae mkao wa kula kupokea kilicho bora,” alisema.

Alisema wimbo wake ameupika katika studio za Asset, chini ya mtayarishaji mahiri, Hizam Hashimu, aliyewahi kufanya kazi na wasanii wakubwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.