Kisandula amlilia bosi wa ‘Ntamba Band’

Dimba - - Jumapili - MWANDISHI WETU

MSANII wa filamu nchini, Omari Kisandula ‘Spoiler’, amemlilia bosi wa Bendi ya Ntamba, Dk. Ntamba na Mungu, kwa kitendo chake cha kuipa kisogo sanaa ya maigizo na kujikita kwenye muziki.

Kisandula aliyewahi kutamba na filamu ya Jinamizi, aliyowashirikisha wasanii wakubwa kama Slim Omari na King Majuto, alisema kitendo cha Dk. Ntamba kuachana na masuala ya filamu, kimemrudisha nyuma sana kwani alikuwa msaada mkubwa kwake kipindi cha nyuma.

“Kazi zangu nyingi nilizofanya nilikuwa nasimamiwa na Dk. Ntamba, sasa tangu ajiingize kwenye masuala ya muziki nimekosa msaada hivyo ningependa kumwomba arudi kwenye filamu kwa ajili ya kutusaidia vijana wake,” alisema Kisandula.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.