Ben Pol aula Ufaransa

Dimba - - Jumapili - NA JESSCA NANGAWE

MKALI wa R&B, Benard Paul ‘Ben Pol’, amefanikiwa kuchaguliwa kuwa balozi mpya wa taasisi ya Maua Associations ya nchini Ufaransa ambayo itamtambulisha rasmi Novemba 18 mwaka huu. Ben Pol ambaye yupo jijini Paris, amesema amekwenda nchini huko baada ya kuitwa kuhudhuria hafla hiyo maalumu iliyoandaliwa na taasisi hiyo ambapo itaambatana na utambulisho wake kama balozi mpya.

Alisema sherehe hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi hiyo kwa lengo la kutoa usaidizi wa kiafya kwa watoto na vijana ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao.

“Maua Associations ni taasisi inayoundwa na kusajiliwa nchini Ufaransa, kwa ajili ya kutoa usaidizi kwa watoto na vijana ili kuwasaidia katika kutimiza ndoto zao na mimi nashukuru kupata nafasi hii kama balozi,” alisema Ben Pol.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.