TETESI ZA MASTAA ULAYA

Dimba - - Jumapili -

COUTINHO: PSG? SITAKI, NAKWENDA BARCA

KIUNGO wa Liverpool, Philippe Coutinho (25), ameuambia uongozi wa klabu hiyo, atakataa ofa yoyote itakayoletwa na PSG kwa ajili yake. Coutinho amedai kuwa mawazo yake ni kujiunga na Barcelona, siku akiondoka Liverpool na si klabu nyingine.

JUVE YAPIGA HODI KWA BELLERIN

JUVENTUS wametuma wawakilishi wake kuzungumza na beki wa kulia wa Arsenal, Hector Bellerin. Bellerin, pia yuko kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu ya Barcelona, hivyo Juventus wanaweza kukutana na ugumu katika zoezi la kuinasa saini yake.

MORATA: NIKO TAYARI KUREJEA MADRID

STRAIKA Alvaro Morata (25), amesema atakuwa tayari kurejea tena Real Madrid, kama mabingwa hao wa Ulaya, watakuwa tayari kumsajili. Morata aliuzwa na Madrid, kwenda Chelsea, miezi minne iliyopita, lakini straika huyo wa Kihispania, amekiri kuwa atakuwa tayari kupokea ofa hiyo.

MOURINHO AMUWEKA LUKE SHAW SOKONI

MANCHESTER United wako tayari kumpiga bei, Luke Shaw, katika majira ya baridi, endapo watapokea ofa kuanzia pauni milioni 20. Kocha wa United, Jose Mourinho, anaamini kuwa wakati wa usajili wa dirisha dogo, Januari mwakani ndio wakati sahihi wa kumuuza beki huyo ili kupata fedha za kutosha za kusajili mlinzi mwingine.

POCHETTINO AANZA KUMBOMOA MOYES

KOCHA wa Tottenham, Mauricio Pochettino, amethibitisha kumfuatilia kwa karibu kiungo mchezeshaji wa West Ham, Manuel Lanzini. Pochettino yuko kwenye mipango ya kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya michuano ya Ulaya, msimu huu.

MASCHERANO AINGIA KATIKA RADA ZA PSG

WABABE wa Ligue 1, PSG, wamemuweka kwenye rada zao, beki wa Barcelona, Javier Mascherano. PSG wanaamini uzoefu wa Mascherano utawasaidia kwenye michuano ya Ulaya, hivyo wanataka kuona kama kuna uwezekano wa kumng’oa, Camp Nou.

ALCANTARA AITEGA BAYERN MUNICH

KIUNGO wa Bayern Munich, Thiago Alcantara, amesema kuwa anayafurahia maisha ya Ujerumani, lakini yuko tayari kurejea Barcelona, kama akihitajika. Alcantara alitua Munich, mwaka 2013 na kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha wababe hao wa Bundesliga.

ATLETICO YAPIGA HESABU KALI KWA HERRERA

KLABU ya Atletico Madrid, imeonyesha nia ya kuihitaji huduma ya kiungo wa Manchester United, Ander Herrera. Herrera anamaliza mkataba na United mwishoni mwa msimu huu, hivyo Atletico wanaangalia uwezekano wa kumshawishi kiungo huyo asiongeze mkataba mpya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.