ULIZA UJIBIWE, UKURASA.

Dimba - - Jumapili -

SWALI: Naomba kujua ni klabu gani ya soka inaongoza kwa utajiri duniani? Ameuliza David Kapaya wa Dumila, Morogoro. 0754979474.

JIBU: Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni kabisa uliofanywa na jarida la Fobes, Manchester United ndiyo klabu inayotajwa kuwa na thamani kubwa ya utajiri duniani kwa sasa, ikiwa na kiasi cha thamani ya pauni billionI 2.86. Hii ni mara ya kwanza kwa United kuongoza orodha hiyo katika miaka mitano.

Barca wako katika nafasi ya pili wakiwa na thamani ya pauni bilioni 2.82, huku mabingwa wa Ulaya, Real Madrid wakishika nafasi ya tatu kwa thamani ya pauni bilioni 2.77.

SWALI: Ndugu Mhariri wa gazeti la michezo na burudani la DIMBA. Nawapongeza wahariri wote wanaohusika katika kuliandaa. Mimi nina maswali mawili. Moja, naomba unipe historia ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), lilianza mwaka gani na lilikuwa chini ya nani? Swali la pili, makao makuu ya FIFA kwa sasa yako Uswisi, je, kabla ya kuwepo huko yalikuwa nchi gani? Mimi ni Saidi Barijongo wa Chavai Kondoa, safarini Arusha na Kahama, Tanzania. 0685369305.

JIBU: FIFA ilianzishwa mwaka 1904 mjini Paris, Ufaransa likiwa chini ya Rais wake wa kwanza ambaye ni Mfaransa, Robert Guerinna. Hadi hivi sasa lina jumla ya nchi wanachama 211, huku lugha rasmi ya Shirikisho hilo ikiwa ni Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani na Kihispania.

Makao makuu ya FIFA yalianzia Rue Saint Honoré, jijini Paris, Ufaransa kuanzia mwaka 1904 kabla ya kuhamia Zurich, Uswisi mwaka 1932.

SWALI: Kabla ya kuibukia Simba na baadaye Yanga, straika Ibrahim Ajib alianzia kucheza soka katika klabu gani? Ameuliza msomaji mwenye simu namba 0757797590.

JIBU: Ajib alianza kucheza soka la ushindani katika kikosi cha timu ya Boom FC ya Ilala, kilichokuwa kikishiriki Ligi Daraja la Pili na la kwanza, kabla ya kutua Simba B, Simba A, kisha kuhamia Yanga.

SWALI: Mimi ni msomaji mkubwa wa gazeti linaloongoza kwa habari za michezo na burudani la DIMBA. Swali langu ni kwamba, ukiacha timu za Liverpool, Manchester United na Chelsea, kuna timu nyingine za England zilizowahi kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya? Kama zipo ni ngapi na zipi? Anauliza shabiki wa timu za Simba na Manchester United, Rama Dibuma wa Morogoro Mjini. 0718111161.

JIBU: Timu nyingine za England zilizowahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ni mbili ambazo ni timu ya Daraja la Kwanza Nottingham Forest, iliyowahi kutwaa ubingwa mara mbili katika miaka ya 1979 na 1980, pamoja na Aston Villa pia ya Daraja la Kwanza, ambayo ilitwaa ubingwa mara moja mwaka 1982.

SWALI: Mhariri pole na majukumu. Naomba unifahamishe timu ya Arsenal imetwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England mara ngapi? Naitwa Omari Yusuf niko Tanga. 065731003.

JIBU: Arsenal imewahi kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England mara 13 katika miaka ya 1930–31, 1932–33, 1933–34, 1934–35, 1937–38, 1947–48, 1952–53, 1970–71, 1988–89, 1990–91, 1997–98, 2001–02 na 2003–04.

SWALI: Naitwa Hassan Lupale wa Ifakara, Kibaoni, nauliza timu ya Liverpool ya England imechukua Kombe la Klabu Bingwa Ulaya mara ngapi? 0715104771.

JIBU: Liverpool imechukua taji la Klabu Bingwa Ulaya (sasa Ligi ya Mabingwa Ulaya) mara tano katika miaka ya 1976–77, 1977–78, 1980–81, 1983–84 na 2004–05.

SWALI: Ndugu Mhariri naomba unikumbushe kikosi cha Manchester United kilichocheza fainali ya Klabu Bingwa Ulaya na Barcelona mwaka 2008. Naitwa Mubarack wa Kanai nikiwa Korogwe. 0653443554.

JIBU: Manchester United na Barcelona hazikucheza fainali mwaka 2008 bali zilifanya hivyo mwaka 2009 kwenye dimba la Stadio Olimpico, jijini Rome, Italia na Man United kufungwa mabao 2-0 ambapo kikosi chake kilikuwa: Edwin van der Sar, John O'Shea, Patrice Evra, Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Anderson (Carlos Tevez), Michael Carrick, Park Ji-sung (Dimitar Berbatov), Wayne Rooney, Cristiano Ronaldo na Ryan Giggs (Paul Scholes).

SWALI: Naomba kujua ni mchezaji gani wa Afrika anayeongoza kwa kulipwa fedha nyingi zaidi duniani? Naitwa Mapinda Ndaki wa Chato. 0743458725.

JIBU: Mchezaji anayeongoza kwa kulipwa zaidi ni Mghana Asamoah Gyan, anayekipiga katika klabu ya

XAVI "Binafsi nimechoka, Itakuwa nI Vlgumu kuendelea kucheza, nina uhakika hu utakuwa ni mwaka wangu wa mwIsho kuwa mwanasoka."

Shanghai SIPG ya China, analipwa pauni 227,000 kwa wiki. Anafuatiwa na Yaya Toure (Ivory Coast Manchester City ya Uingereza (pauni 220,000 kwa wiki), huku Mcameroon Samuel Eto'o akishika nafasi ya tatu kwa kulipwa kitita cha pauni 170,000 katika klabu ya Antalyaspor ya Uturuki.

SWALI: Naitwa Andrea, napatikana Kitunda Saccos, swali langu ni kwamba, Simba ilicheza na timu gani hapa Tanzania ikafungwa mabao 4-0 na ilipokwenda ugenini ikashinda 5-0? Hiyo ilikuwa ni mwaka gani na wafungaji wa mabao walikuwa ni akina nani? 0789718545.

JIBU: Ilikuwa ni mwaka 1979 ambapo Simba walifanikiwa kufanya maajabu katika historia ya soka hapa nchini, baada ya kupindua kipigo cha mabao 4-0 walichokipata kutoka kwa Mufulira Wanderers ya Zambia hapa nyumbani na kwenda kushinda mabao 5-0 ugenini nchini Zambia, timu hizo ziliporudiana. Katika mchezo wa marudiano uliopigwa mjini Lusaka, mabao matatau ya Wekundu hao wa Msimbazi yalifungwa na Thuwein Ally Waziri na mawili George 'Best' Kulagwa.

SWALI: Naomba kumuulizia nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kaichezea Yanga kwa muda gani hadi sasa? Naitwa Abdallah Chuvaka kutoka Iringa Mjini.

JIBU: Mpaka sasa Cannavaro ameichezea timu hiyo kwa miaka 13 na kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi kwenye kikosi hicho.

Cannavaro aliichezea Yanga mwaka 2000-2003 kabla ya kujiunga na Malindi ya Zanzibar aliyoicheza kwa misimu mitatu. Beki huyo wa Taifa Stars, alirejea Yanga mwaka 2006 na kuendelea kuwa kwenye kikosi hicho hadi hii leo.

Wakati akiwa Yanga, Cannavaro aliwahi kwenda kufanya majaribio kwenye timu ya Vancouver White Caps ya Canada, lakini hakufanikiwa kuichezea hivyo kurejea kwenye kikosi hicho. Cha kushangaza ni kwamba, wachezaji wengi aliocheza nao Cannavaro kwenye miaka yake ya kwanza Yanga karibu wote wameshastaafu soka, lakini yeye bado anadunda na ana namba kwenye kikosi cha Taifa Stars.

SWALI: Naomba unikumbushe baadhi ya wachezaji waliowahi kuichezea Nyota Nyekundu enzi hizo ikishiriki Ligi Daraja la Kwanza wakiwamo wachezaji kama Rosta Ndunguru na Ayubu Mzee. Mimi Abbasi Saidi Kunghumwilu wa Temeke, Dar es Salaam. 0713625272.

JIBU: Baadhi ya wachezaji waliowahi kuichezea Nyota Nyekundu miaka hiyo kwa nyakati tofauti ni pamoja na: Stephen Nemes, Sheikh Abdallah, Mohammed Nyauba, John Bosco, John Mngazija, Abunu Issa, Rashid Kipara, Rafael Mapunda, Haruna Macho, Pazi Ally, John Manyama, Stephen Chibichi, Ayoub Mzee, Hamis Dilunga, Mwimbage Omar, Faustine Kibingwa, Roster Ndunguru, Frank Damian, Habib Kondo, Frank Kasanga Bwalya na Zonte Mahundu (Meneja Zonte).

SWALI: Naulizia winga wa Yanga, Simon Msuva, alitokea timu gani kabla ya kutua Jangwani na kisha kwenda kucheza soka nchini Morocco? Ameuliza msomaji mwenye simu namba 0717276826.

JIBU: Msuva alitua Yanga mwaka 2012 baada ya kusajiliwa kutoka Moro United alikokuwa akicheza kipindi hicho, amecheza Yanga hadi mwezi Juni mwaka huu alipoamua kutimkia katika klabu ya Difaa Al Jadid ya Morocco anakocheza hadi hivi sasa.

SWALI: Naomba kuuliza waliko wachezaji hawa: Nteze John (Lungu) na Said Sued Scud. Naitwa Marwa Choma Jeshini Mwanza. 0785165226.

JIBU: Nteze John Lungu kwa hivi sasa yuko nchini Marekani ambako anaishi na familia yake baada ya kustaafu soka ingawa inasemekana kwamba kwa hivi sasa yeye ni Mchungaji. Kwa upande wake, Said Sued Scud yeye baada ya kustaafu soka kwa hivi sasa anaishi mkoani Kigoma akiendelea na shughuli zake za kibiashara pamoja na ufugaji.

Wachezaji wa timu ya Manchester United

ULIZA UJIBIWE

Emmanuel Malima

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.