NI CHIRWA AU AJIB?

Tuzo ya mchezaji bora Oktoba...

Dimba - - Jumapili - NA JESCA NANGAWE

STRAIKA wa mabingwa mara 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Obrey Chirwa, ametajwa kuwa mchezaji bora wa Oktoba akiwagaragaza wapinzani wake, Ibrahim Ajib na Erasto Nyoni.

Kutoka kwa taarifa hiyo ya ushindi wa Chirwa, kuliibua hisia tofauti kwa wadau wa soka, ambapo baadhi waliunga mkono wakisema kuwa alistahili, lakini wengine wakipinga kuwa amependelewa.

Uko upande uliosema kuwa tuzo hiyo ilistahili kwenda kwa Erasto Nyoni, kutokana na mchango alioutoa kwa klabu yake, lakini alinyimwa kwa sababu TFF waliamua ‘kubalansi’ mambo kwa kushindwa kumpa tuzo hiyo mchezaji wa Simba, mara mbili ndani ya miezi mitatu.

Ikimbuke kuwa straika wa Simba, Emmanuel Okwi, ndiye aliyekuwa wa kwanza kubeba tuzo hizi baada ya kung’ara ndani ya Agosti.

Lakini upande wa pili ulidai kuwa Ajib ndiye aliyestahili kubeba tuzo hiyo na si Chirwa, ila amenyimwa na kamati ya TFF kwa madai ya kuogopa ‘kuzidi kumpa sifa’ nyota huyo.

Hoja hiyo ilisindikizwa kuwa taarifa ya ushindi wa Chirwa kutoka TFF, ilikuwa na maelezo mengi yaliyolenga zaidi kumsifia Mzambia huyu, tofauti na ile ya mwezi Septemba alipotangazwa beki wa Singida United, Shaffik Batambuze.

Baada ya mabishano hayo, DIMBA tulipitia kwa makini takwimu za watatu hao ndani ya Oktoba na kuangalia hoja za kila upande ili kujua ukweli wa mambo ulivyo. Takwimu za Chirwa

Oktoba, Obrey Chirwa alifunga mabao matatu katika mechi tatu mfululizo ugenini dhidi ya Kagera Sugar na Stand ugenini na mmoja wa nyumbani dhidi ya watani wao, Simba SC.

Mzambia huyu pia alitoa asisti mbili za mabao kwenye michezo miwili ya ugenini dhidi ya Kagera na Stand United. Straika Ibrahim Ajib ndiye aliyehusika katika kuikwamisha kimiani pasi hizo za Chirwa. Kwa upande wa nidhamu, Chirwa kwa Oktoba, alicheza michezo yote mitatu na kuonyeshwa kadi moja ya njano, aliyoipata kwenye pambano dhidi ya Kagera Sugar. Kwanini alistahili?

Licha ya kufunga kwenye michezo mitatu mfululizo na kuasisti mabao mawili, sababu kubwa inayotajwa kumbeba straika huyu hadi kubeba tuzo hii, ni uwezo wake aliouonyesha kwenye mechi ya watani, dhidi ya Simba.

Lakini pia kipengele cha kutokuwa na kadi kinatajwa kumbeba Chirwa kwa maana ya nidhamu yake kuwa juu kulinganisha na wapinzani wake. Kwanini hakustahili?

Wadau wa soka wanadai kuwa kama kigezo cha kufunga kwenye michezo mitatu mfululizo, mwezi Septemba, straika wa Mbao,Habib Kiombo, alifanya hivyo lakini hata kwenye tatu bora hakuingia. Takwimu za Erasto Nyoni

Huyu ni beki wa kulia wa Simba, hivyo kwa nafasi yake hakufanikiwa kufunga bao lolote kwenye mechi tatu alizocheza Oktoba.

Lakini Nyoni alikuwa msaada mkubwa ndani ya mwezi huu kwa kusaidia mabao manne, akitoa asisti mbili dhidi ya Njombe Mji na moja dhidi ya Yanga, huku rafu aliyochezewa dhidi ya Mtibwa, ilimsaidia Emmanuel Okwi kufunga bao la kusawazisha.

Kwa upande wa nidhamu, Nyoni alimaliza michezo yote ya Oktoba bila kuwa na kadi ya njano. Kwanini alistahili?

Kwa kutazama hali ilivyokuwa mwezi Septemba, beki wa kushoto wa Singida United, Shaffik Batambuze, alibeba tuzo hiyo kwa msaada alioutoa kwa klabu yake, hivyo Nyoni alistahili kwa kubeba tuzo hii kwa asisti zake zilizoipa Simba zaidi ya pointi 5. Kwanini hakustahili? Kwa kuwa Nyoni ni beki, hivyo huenda kamati ilianza kuangalia jukumu lake la msingi uwanjani kwa kupima ni namna gani aliisaidia Simba kutoruhusu mabao mengi.

Kwa Oktoba, Simba iliruhusu mabao matatu dhidi ya Stand Utd, Mtibwa na Yanga, hivyo inaonekana hakufaya majukumu yake kwa asilimia zote. Takwimu za Ajib

Straika huyu aliyetua Yanga msimu huu akitokea Simba, alifunga mabao matatu kwenye mechi mbili kati ya tatu alizocheza, ndani ya Oktoba. Moja dhidi ya Kagera Sugar na mawili dhidi ya Stand United. Ikumbuke kuwa mabao yote aliyafunga katika viwanja vya ugenini.

Lakini Ajib, aliasisti bao moja ndani ya Oktoba lililofungwa na Obrey Chirwa, Yanga walipoichapa Kagera Sugar, mabao 2-1.

kwa upande wa nidhamu, Ajib alipata kadi mbili za njano dhidi ya Kagera na moja dhidi ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC. Kwanini alistahili?

Wadau wa soka wanadai kuwa Ajib alikuwa na msaada mkubwa katika kikosi chake cha Yanga, kwa kufunga mabao ya uwezo binafsi yaliosaidia kuamua mechi.

Lakini pia walimtaja Ajib kama mchezaji hatari zaidi katika safu ya ushambuliaji ya Yanga, akiwa na uwezo wa kutengeneza nafasi za mabao, kama alivyotengeneza pasi kwa Mwashiuya, aliyeasisti bao la Chirwa.

Sababu ya tatu iliyotajwa katika kuonyesha kuwa Ajib alistahili kubeba tuzo hii ni mchango alioutoa kwa Yanga, hadi kufanikiwa kuwepo kwenye tatu bora ya tuzo hizi kwa miezi miwili mfululizo. (Septemba na Oktoba) Kwanini hakustahili?

Inatajwa kuwa kucheza chini ya kiwango katika pambano la watani wa jadi dhidi ya Simba, kulimuangusha Ajib kwa kuonekana hawezi kung’ara kwenye mechi kubwa. Lakini pia kadi mbili alizopata ndani ya Oktoba zilimfanya straika huyu kuonekana hana nidhamu. Kamati inasemaje?

DIMBA tuliamua kuitafuta Kamati iliyoteuliwa na TFF kwa ajili ya kutoa tuzi hizi, ambapo tulifanikiwa kuzungumza na mmoja wa wajumbe wake, mwanahabari, Gift Macha, aliyeeleza vigezo walivyotumia kumpata Chirwa.

“Tunaangalia vitu vingi ikitokea wachezaji wamelingana na hapa ndipo tunapogundua kuwa nani anamzidi mwingine. Kwa Oktoba, walioingia tatu bora ni Ajib, Nyoni na Chirwa, Maoni ya wataalamu DIMBA tulisogea mbele zaidi kwa kukusanya maoni ya wachambuzi na makocha, ambao nao walikuwa na mawazo tofauti katika ishu hii. Mecky Mexime Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, kwa upande wake anaamini Chirwa alistahili kutokana na takwimu na uwezo wake kwa mwezi uliopita. “Sisi ndio wenye jukumu la kuchagua mchezaji mwenye uwezo na tuliona uwezo wa Chirwa ndio sababu tukamchagua,” alisema Mexime akisisitiza kuwa walitumia zaidi takwimu na si porojo za vijiweni. Ally Mayay Kwa upande wa mchambuzi wa soka nchini, Ally Mayay, alisema pamoja na kiwango kizuri alichokionyesha Ibrahim Ajib, bado Obrey Chirwa alimfunika kutokana na mchango wake ndani ya klabu yake. Amesema ndani ya Oktoba, Chirwa alifanya vizuri licha ya Ajib kuweza kuipatia Yanga ushindi wa pointi tatu katika baadhi ya michezo ya ligi kuu kitu ambacho kiliongeza ushindi kwake. “Katika utoaji wa tuzo vitu vingi vinaangaliwa na kikubwa ikiwa mchango wa mchezaji ndani ya timu, inawezekana Ajib ameisaidia Yanga kupata pointi tatu kwa kuweza kuifungia lakini ukimwangalia mwenzake Chirwa naye aliweza kucheza vizuri na ndio sababu iliyoweza kumpatia ushindi,” anasema Mayay. Aliongeza kuwa kigezo kingine ambazo kimekuwa kikizingatiwa na kamati ya tuzo kimechangiwa na nidhamu, ambapo katika michezo aliyocheza Ajib ameweza kupata kadi mbili za njano huku mwenzake Chirwa akiwa kapata moja. Kennedy Mwaisabula Naye kocha mkongwe nchini, Kennedy Mwaisabula ‘Mzazi’, alisema hana tatizo na mshindi wa tuzo kwa kuwa kamati hutazama mambo mengi katika kupatikana kwa mshindi, lakini alishindwa kufafanua sana kwa kuwa yeye ni miongoni mwa wanakamati waliomtangaza Chirwa. “Nadhani sina mengi kuhusiana na tuzo hiyo kwa kuwa mimi ni miongoni mwa waliohusika katika kupitisha mshindi, kikubwa vigezo vilizingatiwa na ndio maana ilienda kwa mchezaji husika.”. Joseph Kanakamfumu Joseph Kanakamfumu alikuwa tofauti kidogo na wachambuzi wenzake baada ya kusisitiza kuwa Ibrahim Ajib alistahili tuzo. Kanakamfumu alisema kwa viwango vya kila mmoja kuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga, aliona Ajib alistahili zaidi kwa kuwa amekisaidia zaidi kikosi hicho hadi kufikisha idadi ya pointi walizonazo hadi sasa huku wakifukuzana na watani zao Simba. “Naona hapa kila mmoja alikuwa na mchango wake ndani ya timu, lakini karata yangu ningeipeleka kwa Ibrahim Ajib. Alikuwa na mchango zaidi ya Chirwa kwenye klabu yao lakini kamati nayo ina vigezo vyake, hivyo ni vyema tukaviheshimu na kuridhika na maamuzi waliyoyatoa.”

“Sisi ndio wenye jukumu la kuchagua mchezaji mwenye uwezo na tuliona uwezo wa Chirwa ndio sababu tukamchagua,”

tuliwapambanisha katika kila takwimu na mchango wao kwa klabu zao,” alieleza Gift.

hivyo

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.