NYOTA ZETU

Dimba - - Jumapili - Utabiri yakinifu kwa Maalim Kombo Shaaban Kombo, simu namba 0710 779 941/ 0686 029 444

MSHALE (SAGITARIUS) NOVEMBA 23-DESEMBA

Ni kipindi chako cha kushinda, ni kwa jambo lolote wenye nyota hii watajikuta wakipewa heshima wasiyoitarajia, kama unahitaji kupanga mipango ya maisha, uchumba au kutafuta kazi au ombi lolote usiache kipindi hiki kikapita.

MBUZI (CAPRICON) DESEMBA 22-JANUARI 20

Utalazimika kufanya jambo zito ili mambo yako yakae sawa, uzito wowote utakaokutokea usikurudishe nyuma, pambana kwa kila hali, hiki ni kipindi chako cha mafanikio na endapo utaona mambo yanazidi kuwa magumu, tafuta ushauri kwa waliokuzidi maarifa.

NDOO (AQUARIUS) JANUARI 21-FEBRUARI 19

Jambo unalolifanya mara tatu halikai vizuri usilirudie tena, weka akiba ya kusamehe na kuachana na lililoshindikana, zipo dalili za kupata aibu kutokana na kung'ang'ania jambo moja, wiki hii unatakiwa kuwa makini zaidi, kwani jambo lolote ulilo na wasiwasi nalo usilijaribu.

SAMAKI (PISCES) FEBRUARI 20-MACHI 20

Moyo wako utakuwa wenye wasiwasi mwingi, pengine unaweza hata kuacha kufanya mambo yako muhimu, kinachokutokea ni uadui unaozuia kufanikisha mipango yako, epuka ushauri wa mtu usiyemuamini, endapo utafanya safari itakuwa yenye mafanikio makubwa.

PUNDA MACHI 21-APRILI 20

Masuala ya mahusiano yatakuharibia mawazo yako muhimu, ukiweza jizuie au yakwepe mambo yoyote yanayohusu mapenzi, hasa kwa mtu usiyekuwa naye karibu sana, dalili zinaonyesha kuwapo nia ya kutaka kukuharibia jambo fulani au kukuongezea mzigo katika mihangaiko yako.

NG'OMBE (TAURUS) APRILI 21-MEI 21

Msaada wako sasa utahitajika kwa hali na mali, usikimbie majukumu, bali ujitahidi, kwani zipo riziki zinazokusogelea kwa karibu, endapo wiki hii utaomba mkopo au jambo lolote la mahitaji yako, utasumbuliwa sana, lakini baadaye utafanikiwa.

MAPACHA (GEMINI) MEI 22- JUNI 21

Kelele zitawasumbua wenye nyota hii, lawama na wakati mwingine kukabiliwa na usumbufu ni vizuri ukajiweka sehemu usizojulikana sana kuepuka usumbufu, pia utegemee kufuatwa na kuombwa mikopo na watu utakaowaonea aibu, jaribu kuwa mkweli kuepuka aibu.

NGE (SCORPION) SEPTEMBA 24-OKTOBA 22

KUNA jambo litakupa faida ambayo hukuitegemea, jitahidi kuwa karibu na familia kipindi hiki ili kuepuka lawama zinazoweza kukuletea mikosi, siku za Jumamosi na Jumatano zina bahati kwako kwa kujaribu jambo gumu lililokushinda.

MIZANI (LIBRA) SEPT 23 OKT 22

Unahitaji kunasuliwa kutoka hapo ulipo, mambo yako yanazidi kukwama, njia ya kujiondoa hapo ni kufupisha mahusiano ya tamaa na unayotaka kujiingiza, itatokea kutoelewana na watu wako wa karibu, kuwa mpole ni suala la kupita tu.

KAA (CANCER) JUNI 22-JULAI 23

Huu ni wakati wako wa kufanya jambo unalotamani moyoni, uwezo wako kipesa utaongezeka na hali ya mahitaji itakaa vizuri, si vibaya ukatumia muda wako kufurahisha nafsi yako ili usahau machungu yaliyopita, siku za Jumapili zinafaa kupanga mikakati ya maisha, kwani itafanikiwa.

SIMBA (LEO) JULAI 24-AGOSTI 23

Utajikuta mwenye furaha kila wakati wiki hii, matatizo yatakayojitokeza katika kazi ya ndani ya familia wewe hayatakuhusu, lakini utawajibika kama mshauri au msikilizaji, tumia busara na usijiweke kimbelembele kuchangia hoja.

MASHUKE (VIRGO) AGOSTI 24-SEPTEMBA

Baraka ya fedha na kipato itazidi kuongezeka na mipango mingi itakaa sawa, lakini moyo wa kufanya starehe utakuwa mweusi, ni vizuri basi ukafanya mipango yako muda huu, masuala ya familia yaliyopo mbele yako yatafanikiwa na hali itazidi kutengemaa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.