HAPA MWAKE EPL

Usajili utanoga timu zikisajili hivi Januar

Dimba - - Jumapili - LONDON, ENGLAND

WAPENZI wa soka wenyewe wanakwambia kipindi kitamu kwao wakati ligi hazijaanza ni dirisha la usajili. Hawajakosea kabisa.

Inawezekana dirisha la usajili wa majira

ya kiangazi linalofungulwa kabla ya ligi mbalimbali kuanza likaya ni kubwa, ila hata lile la Januari nalo lina utamu wake na linasubiriwa kwa hamu.

Hivi sasa Ligi Kuu England ni moja kati ya zile zilizoingia kweny mapumziko ya siku chache, lakini tayari katika mechi

walizocheza tumeona mapungufu na nguvu za timu zao hasa zile zinazopigiwa upatu wa kutwaa taji la ligi hiyo.

Man City inaonekana kutimia kila idara na ni kama hawatahitaji kuingia sokoni ifikapo Januari mwakani, lakini zinazowafuatia wakali hao hazinabudi kuboresha vikosi vyao.

ARSENAL: MLINDA MLANGO

Je, huu ni wakati sahihi wa kumpumzisha Petr Cech?

Hilo linaweza kuwa pendekezo kali na la kumuumiza kipa huyo, lakini ukweli ni kwamba, ‘The Gunners’ hao wanatakiwa kuanza kufikiria maisha yao yatakuwaje bila ya mkongwe huyo golini, ambaye mara tu msimu utakapomalizika atakuwa na umri wa miaka 36!

CHELSEA: USHAMBULIAJI

Straika Michy Batshuayi, anaweza kuwa mbadala mzuri hasa baada ya kuwaokoa mabingwa watetezi hao katika mtanange wa Ligi Kuu dhidi ya Watford, lakini ukweli ni kwamba, Batshuayi si mshambuliaji ambaye ko- cha Antonio Conte atamtegemea katika harakati zake za kutwaa mataji msimu huu na bila shaka kocha huyo ataingia sokoni Januari kusaka mpachika mabao mahiri atakayekuwa akipokezana na Alvaro Morata.

Washika mitutu wa London, Arsenal, mapema wiki hii waliripotiwa kutaka kumsajili mlinda mlango wa klabu ya Real Madrid, Keylor Navas, ambaye anahusishwa kutakiwa na Liverpool.

Ni usajili mzuri kama wakitia nia ya kweli kwani Madrid wenyewe nao bado wanaendelea kumtamani David de Gea wa Man United, na kama wakimpata Mhispania huyo hawatakuwa na haja ya kubaki na Navas.

LIVERPOOL: ULINZI

Bila

shaka kila mtu alishajua kuwa majogoo hao wanahitaji nini, au nakusingizia mdau? Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, alilazimika kujitoa mhanga na kuanza msimu na safu ile ile ya mabeki aliowatumia msimu uliopita baada ya kumkosa Virgil van Dijk.

Lakini, uamuzi huo unaonekana kumgharimu kwani safu yake hiyo ya ulinzi inaonesha wazi kuwa haitoshi kumpa mafanikio pale Anfield na hana budi kuzama sokoni Januari kuibuka na ‘kitasa’ cha maana.

MAN UNITED: ULINZI

Hili halitakuwa na ubishi. Yule beki waliyemtoa Ureno, Victor Lindelof, ameshafeli England licha ya kwamba United ilitumbua kiasi cha pauni milioni 31 kumnyakua kutoka Benfica.

Kocha wa United, Jose Mourinho, atalazimika kusajili beki mwingine wa kati ifikapo Januari kwani anaonekana wazi kutowaamini akina Chris Smalling na Phil Jones.

Mourinho pia ataitegemea United impe kiasi cha kutosha cha fedha ili aunde tena ‘ukuta’ wa klabu hiyo na kuachana na mfumo wa mabeki watatu alioanza kuutumia baada ya Marcos Rojo kuumia.

TOTTENHAM: WINGA

Ukikitazama kikosi cha Tottenham ni kama kimeenea kila idara ila kuna sehemu moja ya winga ambayo inahitaji mchezaji mwenye uwezo wa hali ya juu. Wachezaji waliosajiliwa hivi karibuni, Clinton N'Jie na Georges-Kevin Nkoudou, wamedhihirisha wenyewe kuwa hawaiwezi kazi, nani wa kutua Wembley? Labda wang’ang’anie kwa winga hatari wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, ambaye wamemfukuzia kwa muda mrefu kidogo.

MOURINHO

WENGER KLOPP GUARDIOLA POCHETTINO

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.