Wachezaji Bara waitibua Zanzibar Heroes

Dimba - - Jumapili - NA MAREGES NYAMAKA

KITENDO cha wachezaji walioitwa kwenye timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes wanaokipiga Ligi Kuu Tanzania Bara kutowasili kwa wakati kikosini hapo kinaonekana kulichukiza benchi la ufundi.

Hatua hiyo imemfanya kocha, Hemed Morocco, kubainisha kuwa kama ikifika hadi Novemba 15, mchezaji ambaye atakuwa hajawasili kambini kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Chalenji nchini Kenya, mwishoni mwa mwezi huu hawatampokea yeyote.

“Wachezaji kutoka Bara kumekuwa na uzito kuwasili kambini, hatua inayotushangaza sisi dawati la ufundi. Tumepanga kufanya maamuzi magumu, lakini yatakayokuwa na nidhamu kwenye timu yetu,” alisema.

Wachezaji kutoka Ligi ya Bara walioitwa ni Abdalah Haji ‘Ninja’, Haji Mwinyi na Matheo Athony wote kutoka Yanga, Adeyum Saleh (Kagera Sugar), Abdallah Kheir (Lipuli), Mohamed Issa (Mtibwa Sugar), Suleiman Kassim (Majimaji) na Kassim Suleiman wa Tanzania Prisons.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.