Walimu kunolewa mpira wa magongo

Dimba - - Jumapili - NA WINFRIDA MTOI

CHAMA cha Mpira wa Magongo Tanzania (TAHA), kinatarajia kuendesha mafunzo ya ukocha kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kuanzia Desemba 3, mwaka huu.

Akizungumza na DIMBA, mkufunzi wa mchezo huo, Alice Ngoro, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ufahamu na kasi ya kuinua vipaji vya mpira wa magongo shuleni, tofauti na hali ya sasa, kwa kuwa ni shule chache zinacheza.

Alisema mafunzo hayo yatakayofanyika katika kituo cha michezo cha JKM Youth Park, yatahusisha pia wachezaji wa zamani ambao wataanzia ngazi ya awali kwa kuwapa msingi wa ukocha.

“Mchezo wa magongo bado unahitaji makocha kwa sababu waliopo ni wachache, hivyo chama kimeona njia pekee ni kutoa mafunzo ya ngazi tofauti tofauti kuanzia awali hadi ya juu,” alisema Alice.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.