Miamba saba netiboli kushuka dimbani leo

Dimba - - Jumapili - NA GLORY MLAY

MIAMBA saba wa mchezo wa netiboli wanatarajiwa kuumana leo katika mwendelezo wa Ligi Daraja la Pili, itakayochezwa kwenye Uwanja wa JK Park, jijini Dar es Salaam.

Ligi hiyo imeanza kutimua vumbi juzi, ikishirikisha jumla ya timu 11 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Simiyu na Pamoja Youth, huku Zimamoto wakivaana na Bandari Queens na mchezo wa tatu utawakutamisha Chemchem ambao watacheza na Cocacola Kwanza.

Zimamoto itashuka tena dimbani katika mchezo wao wa pili dhidi ya Magereza, huku Vingunguti wakichuana na Pamoja Youth na mchezo wa sita watacheza Polisi Sengerema na Simiyu.

Mchezo wa mwisho ambao utakuwa unasubiriwa sana kwa hamu na mashabiki utakuwa kati ya Sedico na Cocacola.

Akizungumza na DIMBA jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Judith Ilanga, alisema ligi ya msimu huu imefanikiwa kupata timu nyingi zenye ushindani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.