WINGA MPYA CHAGUO LA YANGA NI HUYU HAPA

Dimba - - Mbele - NA CLARA ALPHONCE

KOCHA Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amewaambia viongozi wake anataka aipe timu yake ubingwa kwa mara ya nne mfululizo, lakini akawapa mapendekezo yake katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Moja ya mapendekezo yake ni kutafutiwa winga mmoja wa kushoto mwenye kasi kubwa zaidi ya ilivyokuwa kwa Simon Msuva, lakini pia mwenye sifa nyingine ya kumudu kucheza kama kiungo wa kati.

Licha ya kuwa mawinga kama Geofrey Mwashiuya, Emmanuel Martin pamoja

na Pius Buswita, kocha huyo anaona bado kuna kitu kinakosekana, hivyo amependekeza atafutwe mwingine matata.

Habari ambazo DIMBA Jumatano limezinasa zinadai kuwa, hata safari yake ya kwenda nchini Congo ni kwa ajili ya kumtafuta winga huyo, ikizingatiwa kuwa mbali na kutaka kutwaa tena ubingwa, lakini pia kufika mbali katika michuano ya kimataifa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.