TSHISHIMBI SAFI, TAMBWE AREJEA MO AWAITA YANGA MEZANI

Dimba - - Mbele - NA CLARA ALPHONCE

WAKATI Yanga wakihusishwa na mpango wa kuitaka saini ya kiungo wa Simba, Mohamed Ibrahim (MO),

KIUNGO wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi ambaye alikuwa akisumbuliwa na malaria, leo anaanza rasmi mazoezi na wenzake huku furaha kubwa kwa mashabiki wa Yanga ikiwa ni kurejea kwa straika wao mpachika mabao, Amis Tambwe ambaye amerudi rasmi mzigoni.

Tambwe ambaye hajagusa mechi hata moja msimu huu kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimkabili, amerejea mazoezini rasmi, huku Tshishimbi ambaye alikosa mazoezi siku kadhaa naye leo akitarajiwa kuungana na wenzake.

Kurejea kwa Tambwe kutaimarisha safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo ilikuwa ikiwategemea zaidi Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa, nzuri.

DIMBA Jumatano lilishuhudia Tambwe akifanya mazoezi na timu hiyo, huku akipewa programu yake maalumu akiwa chini ya uangalizi wa daktari wa timu hiyo Edward Bavu.

"Tambwe amerejea lakini bado anafanya mazoezi chini ya uangalizi, anaendelea kupewa aina ya mazoezi ambayo yatamfanya arudi katika hali yake ya kawaida na ninaamini haitachukua muda," alisema.

Kuhusu kiungo Mzimbabwe, Thaban Kamusoko, alisema bado hali yake haijakuwa sawa na anaendelea na matibabu ambapo huenda akaukosa mchezo dhidi ya Mbeya City, utakaochezwa mwishoni mwa wiki hii, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.