Victor aifuata ‘Rwanda Open’

Dimba - - Jumatano - NA SHARIFA MMASI

BINGWA mtetezi wa mashindano ya wazi ya mchezo wa gofu yanayofanyika nchini Rwanda ‘Rwanda Open’, Victor Joseph, jana amefunga safari kuelekea jijini Kigali, kushiriki mashindano hayo yanayotarajiwa kutimua vumbi leo, kwa lengo la kutetea taji analolishikilia.

Akizungumza na DIMBA jijini Dar es Salaam, Victor, ambaye ni miongoni mwa Watanzania wanaotamba katika mchezo huo, alisema amejipanga kikamilifu dhidi ya wapinzani na kuwataka Watanzania wamwombee ili akaipeperushe vema bendera ya nchi.

“Mwishoni mwa mwaka jana nilibahatika kushiriki michuano ya wazi kule Rwanda na kubahatika kuipeperusha vema Bendera ya Tanzania.

“Leo hii niko njiani kuelekea Rwanda kwaajili ya kwenda kutetea ubingwa wangu, naamini nitakwenda kufanya vema, kikubwa niwaombe Watanzania waniombee ili nikawawakilishe ipasavyo,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.