Star Times yaja na ‘Mfalme wa Familia’

Dimba - - Jumatano - NA SHARIFA MMASI

KAMPUNI ya Star Media (T) LTD imevumbua ofa maalumu kuelekea msimu wa sikukuu, kwaajili ya wateja wa zamani na wale wapya, watakaopenda kujiunga na huduma zao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano na Masoko, Juma Suluhu, alisema lengo la ofa hiyo ni kutaka kuwasogeza karibu na wateja wao waone namna gani kampuni hiyo inatambua umuhimu wao.

“Kupitia Mfalme wa Familia, wateja wetu watapata fursa ya kutazama vipindi mbalimbali kama filamu, michezo aina tofauti tofauti, ikiwamo soka, kikapu, riadha, judo na mengineyo,” alisema.

Suluhu alisema kuwa, ofa hiyo itakwenda sambamba na punguzo la bei ya king’amuzi chao ambapo awali kiliuzwa Sh 47,000 na sasa kinapatikana kwa Sh 34,000

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.