MBWANA SAMATTA HUYOO BUNDESLIGA

Dimba - - Mbele - NA SAADA SALIM

WAKATI akili za Mtanzania Mbwana Samatta zikiwaza zaidi kucheza soka Ligi Kuu nchini England, anaweza akajikuta akiangukia Ligi Kuu nchini Ujerumani 'Bundesliga' au ile ya Italia 'Serie A', baada ya baadhi ya timu kubwa kuonyesha nia ya kuihitaji huduma yake.

Straika huyo, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya KCR Genk ya nchini Ubelgiji, amekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu yangu asajiliwe na timu hiyo mwaka 2016, akitokea kikosi cha TP Mazembe cha nchini Congo.

Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo, amelithibitishia DIMBA kwamba, baadhi ya timu kubwa nchini Italia na Ujerumani zimeanza kummezea mate mchezaji huyo wa zamani wa Simba.

"Mwazoni akili ya Samatta ilikuwa kucheza Ligi Kuu nchini England, lakini huenda hilo likashindwa kutimia kwa sasa, kwani timu kutoka nchini Italia na hata Ujerumani zimeonyesha nia ya kusajili,” alisema.

Alisema wakala ambaye anamsimamia Samatta, Nicholas Onise, amefanya mazungumzo na baadhi ya timu hizo na hatima ya hayo yote yatajulikana Julai, mwaka huu.

KIMATAIFA

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.