MO Ibrahim akubali kutua Jangwani

Dimba - - News - NA SAADA SALIM

HII inaweza kuwa taarifa nzuri kwa mashabiki wa Yanga, baada ya Jamal Kisongo, ambaye ni wakala wa kiungo fundi wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘Mo’, kutamka wazi kuwa, milango ipo wazi kwa timu yoyote, ikiwamo Wanajangwani hao, kufanya mazungumzo na mteja wake.

Mo Ibrahim, ambaye mpaka sasa anapendwa na mashabiki wa Simba, licha ya kwamba amekuwa akisugulishwa benchi, mkataba wake unaelekea ukingoni mwishoni mwa msimu, lakini Wekundu hao wa Msimbazi hawajaonyesha dalili za kukaa naye meza moja kuhusu mkataba mpya.

Akizungumza na DIMBA jijini jana, Kisongo alisema amesikia taarifa kwamba Yanga wanamhitaji mchezaji huyo na yupo tayari kuzungumza na uongozi wa Wanajangwani hao kama kweli wamedhamiria kuhitaji huduma yake msimu ujao.

"Mimi sijazungumza na kiongozi yeyote wa Yanga juu ya Mo Ibrahim, hizo taarifa za kwamba wanamtaka

"Mimi sijazungumza na kiongozi yeyote wa Yanga juu ya Mo Ibrahim, hizo taarifa za kwamba wanamtaka nazisikia tu mitaani, ila kama kweli wanaihitaji huduma yake waje tuzungumze

nazisikia tu mitaani, ila kama kweli wanaihitaji huduma yake waje tuzungumze.

"Unajua siku zote mazungumzo ndiyo yanayoheshimiwa, sasa mimi nasema timu yoyote inayomhitaji ije mezani, kuliko kusikia tu maneno mitaani, naona kama Simba wamemuwashia taa nyekundu, hivyo tunakaribisha mazungumzo na wengine wanaomhitaji," alisema.

Taarifa nyingine kutoka Yanga zinadai kuwa, wanaweza wakamnyakua kiungo huyo mshambuliaji wakati huu ambao wanashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, ikizingatiwa kuwa, wanazo nafasi tatu za kusajili.

USAJILI

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.