Ngorongoro Heroes kama kawa kama dawa leo

Dimba - - News - NA GLORY MLAY

TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, inatarajia kushuka dimbani leo dhidi ya Mali, katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika, michuano inayotarajiwa kufanyika nchini Niger.

Akizungumza na DIMBA, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Juma Mgunda, alisema kuwa, wachezaji wake wote wako sawa kwa ajili ya mchezo huo, ambao unatarajiwa kuwa mgumu, licha ya kuwa nyumbani.

“Mchezo utakuwa mgumu, lakini tunahitaji kutumia kila mbinu ili kushinda na kujitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele.

“Lengo letu ni kuhakikisha tunawapa raha Watanzania wote ambao wamekuwa bega kwa bega na sisi na raha hiyo ni pale timu itakapofanikiwa kwenda kwenye fainali hizo,” alisema.

Naye Nahodha wa kikosi hicho, Issa Makamba, alisema kuwa, anaamini watashinda mchezo huo, kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya.

Ngorongoro imetinga hatua hiyo baada ya kuiondoa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa mikwaju ya penalti 6-5, baada kutoka sare katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini.

SOKA LA VIJANA

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.