Yanga waingia anga za Simba

Dimba - - News - NA MAREGES NYAMAKA

WAKATI zikiwapo taarifa kuwa Simba wanataka kumrejesha mchezaji wao wa zamani, Marcel Boniventure Kaheza, ambaye kwa sasa anakipiga Majimaji, Yanga nao wamezunguka mlango wa nyuma wakitaka kuwapiga bao watani zao hao wa jadi.

Mkali huyo, ambaye anashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa wafungaji, akiwa na mabao 13, amelithibitishia DIMBA kuwa, kuna baadhi ya viongozi wa Yanga wamekuwa wakimshawishi ajiunge nao.

"Kuna viongozi wa Yanga wamenifuata mara mbili kunihitaji kikosini kwao, nilichowajibu ni kwamba wasubiri niipambanie Majimaji kwanza maana haiko sehemu salama na baada ya hapo tunaweza kuzungumza," alisema.

Alisema kwa sasa masuala ya usajili ameyaweka kando, lengo lake likiwa kuhakikisha anashirikiana na wenzake kuinusuru timu yake ya Majimaji na mkasi wa kushuka daraja.

Aliongeza kuwa, mbali na Yanga, timu nyingine zinazomfukuzia ni Simba, Azam FC, Singida United na Coastal Union, ambazo zote zimemfuata kwa nyakati tofauti kwa ajili ya kufanya naye kazi msimu ujao. Mbali na Marcel, pia Yanga wanafanya kila linalowezekana ili kuinasa sana ya straika wa Lipuli FC, Adam Salamba, kwani taarifa kutoka kwa Wanajangwani hao zinadai kuwa, hawatarajii kuwa na Obrey Chirwa, msimu ujao.

Pamoja na kuwapo taarifa za wachezaji kugoma kucheza kutokana na kucheleweshewa stahiki zao, kuna kundi la vigogo linashughulikia suala hilo, huku lingine likiwa mawindoni kunasa saini za wakali.

"Kuna viongozi wa Yanga wamenifuata mara mbili kunihitaji kikosini kwao, nilichowajibu ni kwamba wasubiri niipambanie Majimaji kwanza maana haiko sehemu salama na baada ya hapo tunaweza kuzungumza,"

KIKUMBO

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.