HARMONIZE

amkingia kifua Sarah wake

Dimba - - Burudani - NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya kuenea kwa skendo kuwa penzi la Harmonize na mpenzi wake wa sasa aitwaye Sarah liko hatarini kuvunjika, msanii huyo ameibuka na kusema ni uzushi mtupu.

Harmonize amesema kwa sasa anachoangalia zaidi ni jinsi ya kuishi maisha ya furaha kwake na kuangalia jinsi muziki wake unavyopiga hatua na si kujibizana na watu mitandaoni.

ìMimi kwa sasa naangalia zaidi muziki wangu umefikia wapi, habari za kuachana na Sarah mara anatembea na fulani hazina nafasi kwangu, kikubwa tunaheshimiana na maisha yanaendelea, ifike mahali watu waheshimu mapenzi ya watu, inatosha,î alisema Harmonize.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.