Amina: Nitamzalia Ali Kiba watoto watatu

Dimba - - Burudani - NA SHARIFA MMASI

MKE wa msanii nyota Afrika Mashariki na Kati Ali Kiba, Amina Rikesh, amesema Mungu akimpa uzima na uhai amepanga kumzalia mume wake watoto wawili au watatu.

Ali, anayeendelea kutamba na wimbo wa ëSeduceí, kwa sasa ana watoto watatu, wa kiume mmoja na wawili wa kike.

Akihojiwa na kituo cha Redio Clouds juzi, Amina alisema mbali na kuitwa mama na watoto wa mumewe huyo, atafurahi zaidi atakapomuongezea Ali Kiba mtoto wa nne na kuendelea kutoka kwake.

ìKatika maisha yangu ya ndoa natamani kumzalia mume wangu watoto wawili au watatu, kuitwa mama ni raha sana, asikwambie mtu,î alisema Amina.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.