KENDALL JENNER

CHAIBUA KASHESHE

Dimba - - Showbiz -

MWANAMITINDO na mtangazaji wa kipindi cha Keeping up with the Kardashian, raia wa Marekani, Kendall Jenner, aliwaacha midomo wazi watu mbalimbali waliojitokeza katika tamasha la filamu lililofanyika Cannes, Ufaransa kwa kuvaa nguo iliyoonyesha kifua chake nje.

Kendall aliibua mjadala kwa wahudhuriaji kutokana na kivazi chake hicho ambacho kiliacha sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi na kufanya kila mtu amtazame alipokuwa akitembea.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 22, aliteka umati wa watu uliokuwa umejitokeza katika tamasha hilo ambalo limekuwa likifanyika kila mwaka nchini Ufaransa.

Kamera nyingi zilikuwa zikimmulika staa huyo alipokuwa akipita katika zulia jekundu wakati akiingia ukumbini hapo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.