WLADIMIR KLITSCHKO KUREJEA ULINGONI

Dimba - - Showbiz -

MKALI wa masumbwi wa uzito wa juu raia wa Ukraine, Wladimir Klitschko, aliyekuwa akishikilia mataji ya WBO, WBA, IBO, IBF na mwenye rekodi ya kushinda michezo 64 na kupoteza mitano, huku 53 ikiwa ni kwa Knock Out, amebadili mawazo yake ya kustaafu na sasa anataka kurudi tena ulingoni.

Klitschko, mwenye umri wa miaka 42, alikuwa moto wa kuotea mbali kabla ya kuanza kupotea, kufuatia kupokea kichapo mbele ya Tyson Fury, Novemba 2015 nchini Ujerumani.

Mara ya mwisho mkali huyo kupanda ulingoni ilikuwa Aprili, 2017, alipopoteza dhidi ya Anthony Joshua na kuvuliwa mikanda ya IBF, IBO na WBA, pambano lililotazamwa na mashabiki 90,000, ambalo lilipigwa katika Dimba la Wembley jijini London.

"Huwezi kusema kamwe hutafanya, mambo yanabadilika.

"Mwangalie Arnold Schwarzenegger, alikuwa mwanamichezo baadaye akawa mwigizaji, mwanasiasa na mfanyabiashara, naweza nikarejea tena ulingoni kwa ajili ya kuchangisha fedha," alisema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha habari cha Kimataifa cha 112.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.