Toronto Raptors yamtimua kocha

Dimba - - Showbiz -

BAADA ya kushindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa nusu fainali ya NBA Kanda ya Mashariki dhidi ya Cleveland Cavalier, timu ya Toronto Raptors, imeamua kusitisha kibarua cha kocha Dwane Casey.

Casey ambaye amekiongoza kikosi cha Raptors kwa mafanikio makubwa msimu huu kwa kumaliza wakiwa kileleni mwa Kanda ya Mashariki katika historia ya timu hiyo, lakini amejikuta akitupiwa virago vyake.

Raptors ambao wamevunja rekodi ya kushinda michezo mingi 'Franchise' kwa kushinda jumla ya michezo 59, waliingia katika hatua ya mtoano ya michuano hiyo ambayo walifanya vizuri na kuondolewa hatua ya nusu fainali.

"Baada ya maridhiano, nimeamua kufanya maamuzi haya kwa ajili ya kupiga hatua nyingine kwa Franchise kama timu.

"Kama timu tunatakiwa kukua na kuzidi kuwa bora ili tuweze kufika hatua nyingine," alisema rais wa klabu hiyo, Masai Ujiri.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.