WATAKAOTEMWA SIMBA HADHARANI

Dimba - - Front Page - NA MWANDISHI WETU

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa kwenye hatua za mwisho kumalizika, tayari majina ya wachezaji sita wa Simba yamevuja kwamba msimu ujao hayataonekana tena mitaa hiyo ya Wekundu wa Msimbazi, kwa madai ya kushindwa kuonyesha uwezo.

Simba ambao wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa misimu mitano mfululizo, wanataka kuwa na kikosi chenye wachezaji wenye uwezo mkubwa msimu ujao.

Wachezaji ambao majina yao yamevuja kwamba huenda panga litawapitia baada ya msimu huu kumalizika, ni beki kisiki Jjuko Murushid, straika Mrundi Laudit Mavugo pamoja na wachezaji Ally Shomari, Jamal Mwambeleko, Emmanuel Mseja pamoja na Juma Luizio.

Taarifa zaidi kutoka Simba zinadai kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, Pierre Lechantre, amesema anataka msimu ujao wachezaji wote watakaokuwa kwenye kikosi hicho wawe ni wale wanaojituma.

Kutokana na hali hiyo, taarifa nyingine zinadai kuwa bilionea wao, Mohamed Dewji 'Mo', amesema yeye mapendekezo yoyote atakayopewa na benchi la ufundi atayafanyia kazi kwani shauku yake ni kutaka kuiona Simba ikichanja mbuga kimataifa zaidi.

"Nadhani msimu ujao Simba itakuwa kali kuliko ya sasa, kwani hata Mohamed Dewji amesema yupo tayari kumwaga fedha za usajili kwani shauku yake kubwa ni kuoina timu yetu ikiwika ndani na nje ya nchi," alisema kigogo mmoja wa Simba.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.