Viporo RBA kupigwa Ijumaa

Dimba - - News - NA SHARIFA MMASI

TIMU mbalimbali zinazoshiriki Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), zinatarajiwa kuendelea na ratiba za michezo ya viporo Ijumaa hii, ili kukamilisha mzunguko wa kwanza.

Katika michezo hiyo ya viporo, timu ya ABC itashuka dimbani Ijumaa hii kuwavaa DB Young Stars, ukifuatiwa na mtanange kati ya Pazi na Jogoo.

Kwa upande wa Jogoo, watakutana na wapinzani wao, ABC, wakiwa nafasi ya 12 kwenye msimamo wa RBA, wamejikusanyia jumla ya pointi 17, zilizotokana na kushinda michezo mitano kati ya 13 hadi sasa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.