Nani ni nani? - 1 Dhambi ya kutelekeza watoto inavyowatafuna wanaume

Dimba - - Burudani za wasani - DIMBA JUMATANO. Na Zainab Iddy kuhatarisha maisha

KARIBU msomaji wa safu ya Filamu za Kibongo, inayokujia kila siku ya Jumatano katika gazeti lako pendwa la Dimba Jumatano.

Leo katika Filamu za Kibongo tunaiangalia kazi nzuri inayokwenda kwa jina la 'Nani ni nani? iliyochezwa na wasanii mabalimbali, wakiwamo Blandina Chagula ‘Johari’ na Mohamed Mwambapa.

Filamu hii inaanza kwa kumwonyesha Mwambapa, anayefanya kazi ya upelelezi akizungumza na mama yake juu ya jukumu jipya alilopewa kazini la kumchunguza mfanyabiashara jiji la Dar es Salaam.

Mama yake anamwambia vizuri, lakini akimtaka awe makini kulingana na jukumu lenyewe ambalo linaweza yake.

Upande mwingine anaonekana Johari akiwa mezani anakula pamoja na wazazi wake, huku baba yake akimuuliza anahitaji zawadi gani baada ya kufanya vizuri katika masomo yake ya chuo.

Johari anamuomba baba yake kumnunulia gari jingine baada ya kulichoka lile alilokuwa nayo. Ombi hilo linaonekana kupita, huku akitakiwa kusema jambo lolote atakaloona litampa furaha maishani mwake.

Siku mbili baadaye anaonekana Mwambapa akigonga katika geti la kina Johari, mara anatoka mlinzi na kumuuliza ana shida gani, ndipo Mwambapa akiwa kwenye mwonekano mchafu anaomba kuonana na wenye nyumba, lengo kubwa ni kuomba kazi ya kutunza bustani.

Wakati Mwambapa akibishana na mlinzi juu ya kuingia ndani, mara anakuja Johari na kuuliza kuna nini, ndipo anapoambiwa kijana huyo mchafu amekuja kuomba kazi.

Johari anamuita Mwambapa na kumuuliza anaweza kazi gani na kujibiwa kutunza bustani za maua na kupamba nyumba, bila kufikiria ametokea wapi anaingia naye ndani na kuwaambia wazazi wake kuwa huyo atafanya kazi za bustani.

Wazazi wa Johari wanakubali na Mwambapa anaanza kazi, lakini akitakiwa kulala hapo hapo kazini, jambo analokubaliana nalo.

Siku zinakwenda, Johari anavutiwa kimapenzi na Mwambapa, hivyo anatumia kila njia kumshawishi, jambo linalofanikiwa na kisha kukolea kwenye penzi la Mwambapa.

Wakati akiendelea na kazi ya utunzaji bustani, pamoja na ku- pamba nyumba, Mwambapa anamdadisi Johari juu ya kazi anavyofanya pamoja na sehemu anazoweka karatasi zake muhimu.

Bila ya kujua lengo la Mwambapa, Johari anamueleza kila kitu na hata kufika hatua ya kumuonyesha karatasi zote muhimu na hapo ndipo Mwambapa anapofanya mchakato wa kuziiba kisha kuzifikisha katika mikono ya sheria.

Baada ya wiki moja, Baba Johari anagundua nyaraka zake zimeibiwa ndani, anawasiliana na watu wake, nao wanampa majibu kuwa, kuna mtu yupo katika familia yake amekuja kumchunguza, kwa hasira anaiita familia nzima akiwa na jazba na kuwapa siku tatu warudishe nyaraka zilizopotea ndani.

Kwa leo tunaishia hapa, tukutane wiki ijayo katika mwendelezo wa filamu hii ya Nani ni nani, ili kupata uhondo mzuri na kuona jinsi wasanii wetu wa Bongo walivyoweza kuvaa uhusika wao. Tukutane Jumatano ijayo hapa hapa

Johari anamuomba baba yake kumnunulia gari jingine baada ya kulichoka lile alilokuwa nayo. Ombi hilo linaonekana kupita...

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.