Gabriel

SILOLIJUA ni kama usiku wa giza, hata kama uko kwenye chumba chako hutoacha kupapasa, ndivyo ninavyomwona huyu dogo anayeamini ipo siku masikio yake yanaweza kupita kichwa. U

Dimba - - Dimba Special - NA GOAL MASHINE

Hiyo haiwezekani, dogo hakuna mtu aliyesema John Bocco si straika bora hapa nchini kwa sasa, lakini asisahau kuwa wapo walioacha manukato pale Msimbazi.

Wapo mastraika waliokuwa na kazi ya kufurahisha mashabiki, tena wengine haina haja hata ya kuwataja maana yake tutaamsha mzuka na kuwaibua wazee ambao muda huu wanataka kupumzika.

Lakini katika wachache waliopita hapo, yupo kijana mwenye nguvu na akili ya kupata bao katika mchezo ambao timu haitarajii kushinda.

Ni Emmanuel Gabrile, Mwakyusa aliyekipiga katika klabu ya Simba kwenye miaka ya 2002 na kuendelea kisha akaisaidia sana timu kuivua ubingwa Zamaleck mwaka 2003.

Huyo alikuwa mtu kweli kweli si mchezo, ni mpambanaji, analijua goli lilikojificha.

Utamu wake sasa huyo alikuwa si mkali kwa mechi za Kibongobongo tu, bali hata mechi za kimataifa straika huyo alikuwa balaa.

Ukitaka habari zake waulize Enyimba alivyowafanya kitu mbaya pale shamba la bibi na kuwafanya viongozi wake baada ya mpira kutafuta kujua jina na uraia wake, walikataa kama ni Mbongo, wakidhani anatokea Ghana.

Pamoja na kwamba chama la Simba lilikuwa lipo kamili kuanzia kocha enzi zile James Siang'a, kipa Juma Kaseja, akina Ramadhani Wasso, Ulimbuka Mwakingwe, Selemani Matola, Boniface Pawassa na wengine lakini mshambuliaji huyo alikuwa ni hatari kupitiliza.

Unapotaja mchezaji na kuamua kumsifia si vibaya lakini usimalize ukadhani kwamba mpishi bora ni mama yako tu wakati hujawahi kula hoteli yoyote!

Dogo acha kufuru Gabriel alikiwa mtu na kama hujasikia mambo yake hebu muulize babu yako bila shaka alikuwepo enzi hizo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.