Kisa Simba, Matola ashikishwa Msahafu Lipuli FC

Dimba - - Dimba Special -

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, kocha wa Lipuli FC ya Iringa, Seleman Matola, alikutana na mkasa wa kushikishwa Msahafu na mabosi zake ili kula yamini kama amepewa maelekezo na viongozi wa Simba ili kupata matokeo dhidi ya timu yake. Matola alipata kashkash hiyo kwenye michezo miwili ya timu yake dhidi ya Simba msimu huu, ambapo katika michezo hiyo yote ilimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Matola aliyewahi kucheza Simba na kupata mafanikio makubwa, aliwatoa hofu viongozi wa timu yake ambao walitaka kumfanyia hivyo katika mchezo wa pili uliofanyika Uwanja wa Samora hivi karibuni, alikataa kufanya hivyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.