Kichuya, Luizio wakiona cha moto

Dimba - - Dimba Special - NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

WASHAMBULIAJI wa Simba walikiona kilichomtoa kanga manyoya kwa beki wa kati wa timu ya Dodoma Combine, Ibrahim Ngecha, kutokana na namna alivyowakaba mwanzo mwisho wa mchezo.

Ilikuwa katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Jumapili katika Uwanja wa Jamhuri, jijini hapa, ambapo Shiza Kichuya na Juma Luizio, kila walipotaka kumpita beki huyo ilikuwa ama mtu abaki au mpira uende.

Mara baada ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Dodoma Combine, Jamhuri Kihwelo, alimfagilia beki huyo kwa kudai ni beki bora kabisa. Mtangenge huo uliisha kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.