Okwi awafunika nyota wote Simba Bungeni

Dimba - - Dimba Special - NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

UNAIKUMBUKA ile ziara ya Simba bungeni hivi karibuni. Basi chukua hii. Straika wa kimataifa wa timu hiyo, Mganda Emmanuel Okwi, ndiye mchezaji aliyeombwa na wabunge wengi kupiga naye picha kuliko mchezaji yeyote wa timu hiyo wakati wakiwa bungeni.

Okwi aliambatana na wachezaji wenzake bungeni ambapo mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, wachezaji wa Simba walitoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge, wabunge walimkimbilia mchezaji huyo wakitaka kupiga naye picha hali iliyompa wakati mgumu.

“Geuka na huku Okwi tupige picha wewe ni Super Star,” alisema Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.